Tuesday, October 15, 2013

BRAZIL KUKIPIGA NA ZAMBIA MUDA SI MREFU

Timu ya taifa ya Zambia, Chipolopolo ndani ya saa moja kutokea sasa wataingia uwanjani kucheza mechi ya kirafiki na timu ya taifa ya Brazil. Mechi hiyo ambayo ni muhimu kwa Zambia ikiwa ni mechi yao ya kwanza kucheza na Brazil ambao ni mabingwa mara tano wa kombe la dunia.

“Tunawaheshimu lakini hatuwaogopi” alisema mmoja wa wachezaji wa timu ya Chipolopolo ambao wako jijini Beijing kwaajili ya mechi hiyo, itakayochezwa saa saba kamili saa za Zambia ambayo ni sawa na saa moja usiku Beijing China, katika uwanja maarufu uliojengwa kama kiota cha ndege.

Huku Chipolopolo ikiwa imetolewa katima michuano ya maandalizi ya kombe la dunia mwaka 2014, Brazil itaingia uwanjani, ikiwa ni mechi muhimu pia kwa katika maandalizi ya michuano ya dunia.

Hata hivyo timu ya Zambia itaingia uwanjani huku wachezaji wake  6 wakishindwa kuhudhuria mechi hiyo kutokana na kuugua na majeraha mbalimbali.

Kwa mujibu wa mtandao wa Times of Zambia, wachezaji hao wanao umwa ni Rainford Kalaba, Stoppila Sunzu, Nathan Sinkala, Collins Mbesuma, Davies Nkausu na Mukuka Mulenga

Hata hivyo daktari wa timu ya Chipolopolo alikanisha kuwaruhusu wachezaji hao kusafiri huku wakiwa wagonjwa.


No comments:

Post a Comment