Monday, August 26, 2013

WAKENYA WAMUUA AFISA MSAAFU WA JESHI KWA MAPANGA


"Alisaidia kuendesha mbuga za Kenya wakati mtoto wa mfalme Prince William alipomchumbia mpenzi wake Kate Middleton"
           
Imeripotiwa kuwa aliyekuwa afisa wa jeshi la Uingereza ameuwawa kwa shambulizi baada ya kundi la watu wasiojulikana kumvamia nyumbani kwake Kenya.

Luteni Kanali David Parkinson, 58(pichani kushoto akiwa na mkewe), aliuawa kwa kukatwa katwa kwa mapanga baada ya kuvamiwa na majambazi ambao pia walikuwa na bunduki walipovunja nyumba mapema jana(jumapili) asubuhi.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Telegraph, mkewe alifanikiwa kutoroka na kujifungia stoo mpaka kundi hilo lilipoondoka. Mama huyo alipotoka stoo ndipo alimkuta mumewe amefariki.

Wawili hao walikutwa jumbani lao eneo la miinuko ya Loldaiga eneo la Nanyuki, Laikipia nchini Kenya.
Kabla ya kuhamia katika eneo hilo, Parkinson aliyekuwa mwanajeshi katika kikosi cha parashuti kwa miaka 30, alisaidia kuendesha mbuga ambayo Duke wa Cambridge na Kate Middleton walipochumbiana, gazeti hilo limeripoti.
Inadaiwa kuwa Parkinson aliteuliwa kuwa kaimu mkurugenzi wa hifadhi ya mbuga ya Lewa baada ya kustaafu kama mwanajeshi.

SOMA ZAIDI . . .
Prince William alitembelea mbuga hizo mwaka 2005 kabla ya kurudi na Kate mwaka mara nyingine tena mwaka 2010 alipomchumbia mpenzi wake wakiwa eneo hilo.

Msemaji wa mtoto wa mfalme wa Uingereza alisema wamwesikitishwa sana kwa kifo cha Parkinson, ambaye walikutana katika mbuga hizo.
Polisi wa Kenya wamedai majambazi hayo yaliondoka na kompyuta (laptop), simu pamoja na vito vya thamani.

Msemaji wa polisi eneo hilo, Bw. Marius Tum aliwaambia waandishi wa habari, “Mkewe ambaye alikuwa amefungwa alifanikiwa kuwatoroka na kujificha kwenye stoo, na baadae kurudi na kukuta mumewe akiwa na majeraha ya kutisha”
Alisema uchunguzi wa mwili wa marehemu utafanywa ilikutambua chanzo cha kifo hicho. Mshukiwa mmoja amekamatwa katika kijiji kilichopo karibu na eneo hilo kufuatia msako mkali uliofanywa na polisi wakishirikiana na mbwa wanaotambua harufu.

Ofisi ya Mambo ya Nje imedhibitisha kifo cha Parkinson.

“Tunafahamu kuhusiana na kifo chake na tuko tayari kutoa ushirikiano na kusaidia familia yake katika kipindi hiki kigumu” alisema msemaji wa Ofisi hiyo.




No comments:

Post a Comment