“Jiji limehalalisha na kufungua vyumba
9 ambavyo vitatumiwa na machangudoa na wateja wao kihalali na kwa usalama
zaidi”
Drive-in
ya ngono imefunguliwa rasmi, Zurich katika mkakati wa kuwalinda makahaba ili
kuhamisha biashara ya umalaya nje ya mji wa Swiss.
Vibanda(pichani kulia) tisa vya ngono vilivyojificha ndani ya uzio mkubwa vimeandalikwa kwaajili ya
wauza miili ‘malaya’ na wateja wao kuanzia leo na kuendelea.
Kuna saini
ndogo inayoonesha muda wa kazi, mwamvuli mwekundu kutambulisha eneo hilo kama
eneo la shughuli hiyo ambalo zamani lilikuwa ni eneo la viwanda magharibi mwa
jiji hilo.
Pamoja
na hayo kuna sharia maalumu zimewekwa(kushoto pichani). Mteja lazima awe na umri usiopungua
miaka 18, mtu mmoja tu kwenye gari, na kondom lazma itupwe kwenye vyombo
maalumu baada ya kutumika.
Kuna
eneo ambalo mteja anaweza kuchagua mwanamke anayemfaa, pamoja na makubaliano ya
bei kabla ya kuelekea kwenye kibanda, ambacho ni cha mbao kinacho fanana na
eneo la kuegesha gari.
Kila
kiboksi kina alamu ili kuwalinda Malaya hao.
Michael
Herzig, mkurugenzi katika huduma ya jamii ya wafanyakazi wa ngono jijini
alisema “Umalaya ni biashara “
“Hatuwezi
kuzuia, hivyo tunataka kudhibiti ili kuwasaidia wafanyakazi wa ngono na jamii,
sababu bila kufanya hivyo uhalifu unaongezeka na wahuni wanazidi kuwa wengi”
Ursula
Kocher, Mkurugenzi wa Flora Dora, mtandao unaounga mkono Malaya, alisema kuwa
machangu doa mara nyingi huchukuliwa na kupelekwa kwenye porini au nje ya mji
na kujikuta katika mazingira hatari.
Alisema
“ hapa wanabakia humuhumu ndani na kuhudumia wateja wao haraka”
Eneo
hilo la drive-in ya ngono limehalalishwa na wakazi wa Zurich katika sharia ya
mwezi machi, 2012baada ya kupigiwa kura kwa asilimia 52.6 kukubaliana nalo.
Eneo
hilo pia lina makubaliano mazuri tu yanayohusisha vyama vyote vya siasa nchini
humo, likiwa na wanachama wengi wa chama cha Swiss People's Party (SVP) wanaopinga
mpango huo.
"haitofanikiwa,
labda kwasababu wateja hawatokuja au eneo hilo halitotumiwa na machangudoa”
alisema Sven Oliver Dogwiler, mwanasiasa wa eneo hilo ambae ni mwanachama wa SVP.
No comments:
Post a Comment