Monday, August 12, 2013

MUGABE ATOA HUTUBA BAADA YA UCHAGUZI


Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe anatarajiwa kutoa hotuba yake ya kwanza tangu kushinda uchaguzi mkuu wa Zimbabwe zaidi ya wiki moja iliyopita.Mugabe atahutubia umma wakati wa sherehe za kuadhimisha siku ya mashujaa mjini Harare kuwakumbuka wale waliofariki wakipigania uhuru wa taifa hilo Chama hicho kimewasilisha malalamiko yake kuhusu uchaguzi mkuu ambao kinasema ulikumbwa na wizi wa kura kikitaka uchaguzi huo kurejelewa.Chama pinzani cha MDC, chake waziri mkuu Morgan Tsvangirai, kitasusia sherehe hizo.

Bwana Mugabe alishinda 61% ya kura kwenye uchaguzi huo uliokamilika tarehe 31 mwezi Julai, huku mpinzani wake Morgan Tsvangirai akichukua nafasi ya pili kwa 35% ya kura zilizopigwa.Chama cha Mugabe Zanu-PF kilishinda wingi wa viti vya bunge kikipata zaidi ya thuluthi mbili ikiwa ni viti 160 ya viti kati ya 210 vya bunge zima.


Sherehe za kuadhimisha siku ya mashujaa Zimbabwe, ni sherehe za kujivunia kwa wazimbabwe wakati ambapo nchi hiyo ilijipatia uhuru wake miaka ya sabini.Hii leo Mugabe atatoa hotuba yake ya kwanza katika eneo la kumbukumbu la vita hivyo na ambako baadhi ya wapigania uhuru wamezikwa.

Hotuba za Mugabe zinasifika zaidi kwa siasa zake kali za kizalendo, na ambazo zaidi hulenga mkoloni wake wa zamani Uingereza na pia anatarajiwa kujipiga kifua kufuatia ushindi wake mkubwa katika uchaguzi mkuu uliopita mwezi jana.

Chama cha MDC kinasusia sherehe hizo katika kile kinachosema ilikuwa wizi mkubwa wa kura uliofanywa na chama cha Zanu-PF, kwa hivyo sherehe hii bila shaka itazongwa na siasa.

Mugabe bado hajaapishwa kwa muhula wake wa saba akitawala Zimbabwe, kwa sababu ya kesi ya MDC mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi huo.

MDC kilisema kina ushahidi wa kutosha kuonyesha kuwa wizi wa kura ulitokea na kwamba kulikuwa na visa vingine vilivyohujumu matokeo ya uchaguzi huo ikiwemo, rushwa , dhuluma na kuvurugwa kwa daftari la wapiga kura.

No comments:

Post a Comment