Monday, August 26, 2013
MENDE MILIONI 1 WATOROKA
Imeripotiwa kuwa mende zaidi ya milioni moja wametoroka kutoka kwa shamba walimokuwa wakifugwa nchini China ili kuweza kutumika kwa dawa za kienyeji.
Mende hao walitoroka katika shamba eneo la Dafeng, mashariki mwa Jiangsu, na kuelekea katika mashamba ya mahindi yaliyopo karibu na eneo hilo. tukio hilo lilitokea mapema mwezi huu baada ya mtu asiyejulikana kuharibu sehemu ambayo walikuwa wanafugwa, gazeti la Modern Express lilisema.
Wakuu wa kudhibiti maradhi wametuma wapelelezi watano katika eneo hilo kutoa mpango wa kuwaondoa.
Mmiliki wa shamba hilo Wang Pengsheng aliwekeza zaidi ya Sh1.3 milioni katika kilo 102 za mayai ya Periplaneta americana baada ya kuunda mpango wa biashara wa miezi sita, ripoti ilisema.
Mende kwa kawaida huchukuliwa kama mdudu lakini wanaoamini dawa za kienyeji za Wachina hutumia mimea na pia wanyama ambao ni pamoja na viumbe vilivyopo hatarini wakisema kuwa vinaweza kutibu kansa, kupunguza uvimnbe na kumarisha kinga maradhi.
Kufikia wakati ambapo kinyumba cha plastiki ambapo walikuwa wakifugiwa kiliharibiwa, kulikuwa na kombamwiko zaidi ya 1.5 milioni waliokuwa wameanguliwa na walikuwa wakilishwa chakula ambacho ni pamoja na “matunda na biskuti” kila siku, Wang alinukuliwa kusema.
Bw Wang alisema kuwa alikuwa ametarajia kutengeza zaidi ya Sh14,000 kama faida kwa kila kilo ya mende ambayo angeuza, lakini sasa anakabiliwa na hasara kubwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment