Thursday, July 18, 2013

MASHAHIDI 3 WAONDOLEWA KESI YA UHURU KENYATTA

Taarifa zilizotufikia hivi punde zimesema kuwa Fatou Bensouda ambaye ni kiongozi wa mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC, amewaondoa mashahidi watatu katika kesi dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya

Bi Bensouda alisema mashahidi nambari 5 na 426 wamefutiliwa mbali ushahidi wao kwa sababu za wasiwasi kuhusu usalama wao.

"kwa kifupi, inaonekana kuwa wasiwasi wa shahidi nambari tano, wameogopa sana kuhusu usalama wao na kuwa athari za kutoa ushahidi wake huenda zikawa na madhara makubwa kwa maisha yake na kwa hivyo akaamua kufutilia mbali ushahidi wake.'' alisema Bensouda kwa ujumbe wake kwa majaji mnamo Jumanne.


Aliongeza kuwa upande wa mashtaka, ulikuwa umefanya mashauriano na shahidi nambari 426 kumtaka abadili msimamo wake, lakini mazungmzo hayakufua dafu.

"upande wa mashtaka umefanya mazungumzo na shahidi 426 kujua ikiwa hatua zozote zinaweza kuchukuliwa kuodnoa wasiwasi wake pamoja na kumwezesha kuhudhuria kesi. Mazungumzo hayo, hata hivyo hayakufua dafu baada ya kusisitiza kuwa hayuko tayari kutoa ushahidi wake, '' aliongeza kusema Bi Bensouda said.

Hata hivyo mwendesha mashtaka aliwaaambia majaji kuwa ushahidi wao sio muhimu tena kwa ushahidi wake dhidi ya mtuhumiwa.

Kesi dhidi ya Uhuru Kenyatta itaanza kusikilizwa Novemba 12.

No comments:

Post a Comment