Nchi ya Uganda inakabiliwa na ukata wa kondomu, hali inayoleta utata juu ya ongezeko la kasi la maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Kwa mujibu wa mganga mkuu wa wilaya ya Masaka Dk. Stuart Musisi, aliweka wazi kuwa wilaya yake haijapewa kondomu kwa karibu miezi miwili sasa hivyo wilaya hiyo ipo kwenye hatari ya ongezeko la kusambaa magonjwa ya zinaa hususani ukimwi.
Alisema wilaya nyingi zimekumbwa na ukata huo huku mahitaji yakiwa ni makubwa ikilinganishwa na kiasi kilichopo.
Alisema wilaya hiyo inahitaji kondomu 600,000 kila baada ya miezi miwili ili kutosheleza mahitaji ya watumiaji lakini katika kipindi hicho imepewa kondomu 1000,000 tu ambazo hazitoshi.
Kwa upande wake Ofisa Mwandamizi wa magonjwa ya kuambukizwa na ukimwi wa wizara ya afya ya Uganda Dk. Shaban Mugerwa, alisema tatizo hilo limetokana na kuchelewa taratibu za ununuzi ambalo liko nje ya uwezo wa nchi hiyo.
Baadhi ya maofisa wa afyakutoka mkoa wa kati wamesema wilaya zilizo katika mkoa huo zimeathirika zaidi baada ya kupata idadi ndogo ya kondomu ambayo haitoshelezi mahitaji.
No comments:
Post a Comment