UTAFITI umebainisha kuwa Wamarekani wengi wameridhia ndoa za jinsia moja, ingawa baadhi yao wamekuwa wakizipinga kwa nguvu zote.
Kwa mujibu wa utafiti ambao ulifanywa na Taasisi ya Pew Research Center hivi karibuni, ulibainisha asilimia 72 ya Wamarekani hawaoni umuhimu wa ndoa za jinsia moja huku asilimia 51 katika tafiti tofauti wakikubali ndoa hizo.
Utafiti huo ulifafanua kuwa kila kundi, ambalo lilikuwa likiunga mkono upande wake katika ndoa hizo lilijiona lenye nguvu na hoja za msingi kuliko lingine.
Mbali na hayo katika uchambuzi wa kitakwimu, kupitia utafiti huo asilimia 42 ya wahojiwa walikiri ndoa za jinsia moja ni kinyume cha sheria wakati asilimia 45 walisema ni dhambi.
Hata hivyo utafiti huo ulizinduliwa juzi nchini Marekani, ambapo taasisi ya Pew iliwahoji watu zaidi ya 1,504 kwa njia ya simu katika majimbo 50 ya Marekani kuanzia Mei mwaka huu.
No comments:
Post a Comment