Tuesday, June 11, 2013

LK 4 WA UGANDA ANG'OLEWA BIG BROTHER THE CHASE


SAFARI ya washiriki kutoka nchini Uganda imefikia mwisho katika mashindano la Big Brother The Chase, baada ya mshiriki LK4 kuyaaga mashindano hayo kutokana na kura zake kutotosha kumbakisha katika jumba.

Katika hali ya kukatisha tamaa zaidi ni pale nchi inapokuwa katika hatari zaidi ya kupoteza washiriki kwenye jumba hilo, ambapo nchi ya Kenya imebakiwa na mshiriki mmoja, anayefahamika kwa jina la Annabel, huku Afrika Kusini kumpoteza mshiriki mmoja ambaye ni Koketso na kubaki katika jumba hilo mshiriki Angelo pekee akiwa anawakilisha nchi hiyo.


Wakati huo huo, kwa upande wa Tanzania Feza Kessy, ambaye alikuwa kikaangoni alipona na kubaki katika jumba hilo baada ya kura zake kutosha kumbakisha.

Kwa upande wa orodha ya wiki hii, Bolt wa Sierra Leone amepona kwa mara nyingine, ambapo wiki iliyopita alipendekezwa kutoka, lakini aliokolewa na kipenzi chake Betty aliyekuwa HOH, lakini tena kwa mara nyingine alipendekezwa kwa kura nyingi, ila ameokolewa tena na HOH wa Diamond Melvinopted ambapo nafasi yake kupewa Annabel.

Mashindano hayo yanaendelea kwa washiriki kupendekeza tena ambao wangependa waingie katika kikaango, kabla ya kupigiwa kura na watazammaji.



No comments:

Post a Comment