Msanii wa muziki wa kizazi kipya Mez B ambaye ni mmoja wa rafiki wa karibu na msanii Albert Mangwea 'Ngwair' aliyebeba picha ya msanii huyo wakiingiza mwili wa marehemu katika kiwanja cha Jamuhuri mkoani Morogoro jana ambapo ndipo heshima za mwisho zilitolewa na wakazi wa morogoro.
Umati wa wakazi wa mkoa wa Morogoro na baadhi ya wasanii wa muziki wa bongo fleva wakiwa wamelizunguka gari lililobeba mwili wa msanii huyo.
Jeneza lililowekwa mwili wa msanii huyo likiwa limebebwa teyari kwa kuzikwa katika makaburi ya kanisani yaliyopo Kihonda mkoani Morogoro
Mmoja wa rafiki wa Ngwair akishikwa alipokuwa analia wakati wa maziko
Mwili wa marehemu ukiingizwa kaburini
Rafiki wa karibu wa msanii huyo M to the P akizuiwa na polisi wakati alipokuwa anaangalia kaburi la msanii huo
Mtayarishaji wa muziki wa kizazi kipya P Funk akishangiliwa na mashabiki wakati alipotoka kumpumzisha msanii Ngwair
No comments:
Post a Comment