Friday, June 07, 2013

BREAKING NEWS: NDOA YA RAIS WA URUSI YAVUNJIKA HADHARNI



Rais wa Urusi Vladimir Putin na mkewe Lyudmila

Rais wa Urusi Vladimir Putin na mkewe Lyudmila waachana rasmi na mwisho wa ndoa yao kuwa wazi rasmi.

Wawili hao, wamekuwa kwenye ndoa kwa miaka 30, walitangaza hadharani kuvunjika
kwa ndoa yao kwenye televisheni ya taifa baada ya kuhudhuria maonesho ya mziki wa balee

‘ni maamuzi ya pamoja, hatuonani, kila mmoja ana maisha yake’ alisema Putin.

Naye mama Putin amekuwa hadimu sana kuonekana hadharani katika miezi ya hivi karibuni, kitendo ambacho kimeleza hisia kwenye vyombo vya habari nchini Urusi.

Anajulikana kwa kutopenda kuonekana, na alimwambia mtangazaji wa televisheni, kusafiri ni kazi ngumu sana kwake.’Vladimir Vladimirovich yeye ni kama kaolewa na kazi yake’ alisema mama huyo.

Talaka hii ni ya “kistaarabu” na wawili hao “wataendelea kuwa pamoja” alisema.
“nina shukuru sana kuwa na Vladimir...na kwamba ataendelea kunisaidia na mapenzi yake kwa watoto, na watoto pia wanaliona hilo,” aliongeza mama Putin.

Nae Rais Putin alidhibitisha hilo kwenye televisheni kwamba wawili hao hawaishi pamoja. “tutaendelea kuwa pamoja nauhakika milele” alisema Putin.

Vladimir Putin na Lyudmila Shkrebneva walifunga ndoa yao mwaka 1983. Wana watoto wawili wa kike, Maria na Yekaterina, watoe wakiwa katika rika la miaka 20.

"watoto wetu wamekua na kila mmoja ana maisha yake," alisema mke wa Putin.
Yeye na Putin walionekana pamoja hadharani kwenye sherehe za kuapishwa Rais Putin katika kipindi chake cha tatu tarehe 7 Mei 2012.

Kwa mujibu wa BBC, taarifa hizi zimepokelewa kwa mshtuko mkubwa kwa raia wa Urusi, ambao hawajazoea kuona viongozi wao wakiachana tena hadharani, pamoja na kwamba Urusi ndio inaongoza kwa ndoa kuvunjika duniani


No comments:

Post a Comment