ATIMULIWA KLABU BILA KUTEGEMEA
Justin
Bieber(JB) kwa uhakika si mtoto tena, sasa hivi ana mashabiki mpaka wengine
wanamtupia brazia (JUU PICHANI) jukwaani. JB mwenye miaka 19 aliweka picha ya kivazi hico cha
ndani cha wanawake kwenye mtandao wa kijamii wa instagram.
Brazia hiyo
ya rangi ya pink ilirushwa na mmoja wa
mashabiki wake juzi jumapili (tarehe 9)
alipokuwa kwenye shoo ya Believe.
JB aliweka picha
hiyo na maelezo yake “I guess everyone grows up” akimaanisha nahisi kuwa kila
mtua anakua.
Wakati
mashabiki wa JB wamekua, gazeti la The Sun limeripoti kuwa msanii huyo
alibadilika rangi ya uso alipotimuliwa kwenye klabu ya kujirusha na maarufu
sana Los Angeles, Marekani iitwayo Lure's Toxic aLuau Beach Party ilipofika saa moja jioni kisa umri mdogo.
Gazeti hilo
lilidai Bieber aligundulika baada ya rapa maarufu The Game kumgundua, ambapo chanzo
kimoja kilieleza kuwa ‘mmoja katika kundi la Justin alitokea mapema na kudai
kuwa Justin angekuja baadae’
‘wenye klabu
wakasema hawatomruhusu kwasababu hana miaka 21. Lakini Bieber alikuja na
kujaribu kuingilia mlango wa nyuma’ kilieleza chanzo hicho na kuripotiwa kwenye
gazeti la The Sun.
Chanzo hicho
kiliendelea ‘The Game alikuwa kwenye mic na ndipo alimuona Bieber akijaribu
kuingia na kusema kwa nguvu Bieber anaingia ndani’
‘ndipo
walinzi walipomuona na kumsindikiza nje mara moja. Akaondoka maramoja huku
akijiskia vibaya’
No comments:
Post a Comment