Friday, May 24, 2013

VIBE RUNWAY KUKUTANISHA WATU MAARUFU


Mbunifu wa mitindo anayekuja kwa kasi, Veronica Lugenzi (Pichani Juu) wa Tanzania kwa kushirikiana na wabunifu wengi kutoka nchi za Marekani, Kenya na Zambia watafanya onesho ya mavazi kwa mara ya kwanza kesho kwenye Ukumbi wa Ledger Plaza Bahari Beach Hotel.

Onesho hilo maarufu kama Vibe Runway litakuwa la kihistoria kwa mujibu wa Veronica kutokana na kushirikisha wabunifu wachanga, wazoefu na wa kimataifa. Alisema wamepanga kuonesha mavazi ya kisasa zaidi katika onesho hilo, huku wakipata burudani ya muziki kutoka kwa wasanii wa hapa nyumbani na wa nchi jirani.

 




Baadhi ya wabunifu maarufu ambao wataonesha mavazi yao ni Asia Idarous, ambaye amepata umaarufu kutokana na onesho lake la Lady in Red na Kanga Za Kale. K a t i k a o n e s h o h i l o lililodhaminiwa na Vayle Springs, TeenSpot Magazine, Gonga Mx Blog, Missie Popular Blog na Ledger Plaza Bahari Beach Hotel, pia litawashirikisha wabunifu wengine wa mavazi kama Kemi Kalikawe, B Designes na VS: VERNIC ambao wote wanatoka Tanzania.
 
Mbunifu kutoka Kenya ni Mohamed Bana na Estelle Mantel ataiwakilisha Zambia na kutoka Marekani (Washington DC) ni Ibrahim Pure. Wanamitindo mbalimbali m a a r u f u w a Ta n z a n i a watakaokuwepo katika onesho hilo ni, Meena Xirs, Rimaly Said Odemba, Miss Universe- Winfrida Dominique, Miss Tanzania anayeshikilia taji la michezo, Mary Chizi, Macrida Joseph, Neema Doreen Sylvery, Rachida Ussuale na Lota Mollel.
 
Pia kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii wa Tanzania, wakiongozwa na mwakilishi wa Tanzania katika Big Brother Africa Julio Batalia na wasanii wengine kama G1, JC, Melisa John, Makjams na King Kapita.

 



No comments:

Post a Comment