Wednesday, April 03, 2013

MATOKEO YAMCHANGANYA DOGO JANJA



MSANII wa muziki wa kizazi kipya Abubakar Chende 'Dogo Janja' amejikuta akijichanganya kutoa maelezo  juu ya kuendelea na kidato cha tatu katika shule ya sekondari Makongo ambao hapo awali alituma maelezo ya kukanusha kufeli mtihani wa kidato cha pili  kupitia mtandao wa kijamii Facebook

Aliamua kutumia mtandao huo kwa ajili ya kukanusha habari yake ambayo imekuwa gumzo kwa baadhi ya mashabiki wake kutaka kujua ukweli wa jambo hilo, Maisha ilipokutana naye msanii huyo alijikuta akijichanganya kwenye maelezo yake

Dogo Janja alisema kuwa anawashangaa watu wanaomuongelea kuwa ameferi mtihani wa kuingia kidato cha tatu wakati yeye anafahamu kuwa hajaferi ingawa kwa kipindi cha mwezi uliopita hakuweza kuhudhuria darasani kwa sababu alikuwa kwenye ziara ya kimuziki nchini South Afrika

Alipoulizwa ili aendelee na masomo yake kidato cha tatu anatakiwa kuwa na wastani wa asilimia ngapi msanii huyo alisema kuwa anatakiwa kuwa na wastani 31 ingawa yeye amepata wastani 27 na anashangaa kupata wastanii huo

Alisema kuwa anashangazwa na wastani huo kwani aelewi umekujaje ingawa hakubahatika kuyaona matokeo yake ya mtihani kwa sababu ambazo yeye hajafahamu alipata taarifa hiyo ya matokeo kupitia uongozi wa shule hiyo

"Mimi sijafeli ila nashangaa kuwa na wastani 27 na matokeo yangu hayakubandikwa sijui kwa sababu gani ingawa si peke yangu ambaye matokeo hayakubandikwa kuna baadhi ya wanafunzi wenzangu nao hajabandikiwa naamini nimefaulu na nataka nilishughurikie hilo swala " alisema Dogo Janja

Alisema kwamba anampango wa kufwatiria ili kujua ukweli kuhusu matokeo yake ndipo atazungumza wazi juu ya swala hilo kwani alikuwa teyari ameshaanza kusoma kidato cha tatu



No comments:

Post a Comment