Wednesday, December 12, 2012

WASANII WAJIANDAA KUMPOKEA RAY C




KITENDO alichofanya msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Rehema Chalamila cha kujitokeza na kwenda kutoa shukurani kwa Rais Kikwete kumeibua hisia za tofauti kwa baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya Tanzania

Baadhi ya wasanii wamefurahishwa na kitendo hiko huku wakiamini kuwa ni kitendo cha ushujaa kwa kujua wapi ulipokosea na kurekebisha ili makosa yasijurudie

Akizungumza jijini Dar es Salaam msanii anayekuja kasi katika tasnia ya muziki wa bongo fleva Racher Haule 'Racher' alisema kuwa ujio wa Ray C kwake ni faraja kwani ndoto yake ya kufanya kazi pamoja itatimia

Alisema kuwa kutokana na kurejea kwa msanii huyo kutamletea changamoto katika tasnia ya muziki huku akifikiria kuongeza juhudi ili aendelee kuwa bora zaidi

"Ujio wake ni changamoto kwangu kwa sababu tunaimba miondoko inayo fanana, kwa kipindi chote nilikuwa sina mpinzani hivyo nina faraja kwa ujio wake, nina amini sasa ndio wakati wangu wa kufanya naye kazi niliyoikusudia kuifanya" alisema Racher

Alisema kuwa faraja kubwa aliyekuwa nayo ni kuona msanii anayeshindana naye sasa yupo vizuri na yupo teyari kuingia katika 'gemu' kama alivyokuwa mara ya kwanza

Kwa upande wa Ommy Dimpoz mzee wa pozi kwa pozi alisema kuwa hawezi kumlaumu kwa kile alichokifanya zaidi ya kumpongeza kwa maamuzi aliyofikia kwa kuamua kupokea matibabu ambayo sasa ndio yamemfanya kuwa na nguvu tena

Alisema kuwa msanii huyo alikuwa bado anadeni la muziki kwani muziki bado ulikuwa unamwihitaji na mashabiki pia hivyo sasa ndio wakati wake yeye kujipanga na kuendeleza kazi ya muziki

Ray C ambaye alikuwa anasumbuliwa na maradhi yaliyosababishwa na matumizi ya madawa ya kulevya, pamoja na hayo amekuwa na mchango mkubwa katika tasnia ya muziki nchini hivyo kurejea kwake na kuwa na afya njema kutaleta changamoto katika tasnia ya muziki nchini





No comments:

Post a Comment