Wednesday, December 12, 2012

MOLLEL AJIPANGA KUFANYA KWELI MOZAMBIQUE FASHION WEEK




MSHINDI wa Tuzo ya Ubunifu wa Mavazi Tanzania, Gabriel Mollel ajipanga kikamilifu katika kuwakilisha nchi kwenye maonyesho ya Mozambique Fashion Week 2012 yanayotarajia kufanyika mapema wiki hii.

Mollel ambaye amejinyakulia tuzo mbili ikiwemo mbunifu malidhawa na Mbunifu bora wa kiume katika tuzo za  Swahili Fashion zilizofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na jarida la Maisha alisema kuwa amejipanga kikamlilifu katika kuiwakilisha nchi kwenye maonyesho hayo huku akiwa makini na bidhaa atakazo peleka kwenye maonyesho hayo.

Akizungumzia tuzo hizo alizopokea alisema kuwa,kwake anachukulia ni moja ya changamoto zinazomsababisha kila kukicha nini afanye ili aendelee kuwa bora zaidi.

Alisema kuwa tuzo ni kitu cha heshima na ili aendelee kubaki katika ubora ni lazima uwe na mikakati thabiti inayoambatana na ubunifu wa hali ya juu ili kila siku uweze kuwa tofauti na wabunifu wengine.

Mollel alisema kuwa kikubwa kilichompa ushindi kwenye onyesho la Swahili Fashion Week ni kuingiza bidhaa ndogondogo tofauti na kuwa mbunifu kwa kuwa na machaguo yenye ubora na upekee

"Huwa nakuwa na faraja sana kila mahali ninapotembea na kukutana na watu wamevaa bidhaa zangu tofauti tofauti, hii inanipa uwezo wa kuendelea kufikiria kesho niwe na ubunifu wa hali ya juu ili niendelee kuwa bora," alisema Mollel.

Mbali na hayo, aliongezea kwamba kipaji chake kingeonekana muda mrefu kama angepata ushirikiano na wadau mbalimbali ila amekuwa akisimama mwenyewe mpaka hapa alipo fika.



No comments:

Post a Comment