Friday, November 02, 2012

Mhariri Wa Business Times Apigwa Risasi

Mnaku Mbani (Mhariri wa Business Times ) akiwa amelazwa katika hospitali ya Muhimbili leo asubuhi baada ya kuvamiwa na kupigwa risasi jana akiwa anaelekea nyumbani kwake usiku wa saa mbili jioni. Katika tukio hilo alikuwa na abiria wenzake 6 ambao nao walipigwa risasi na baadhi yao kutolewa na kuruhusiwa. Mnaku alipigwa risasi juu yo mdomo na risasi hiyo kutokea kwenye shavu lake la kushoto, bado yuko chini ya uangalizi wa madaktari. Taarifa zaidi tutaweletea baadae, endelea kufuatilia hapa

No comments:

Post a Comment