Thursday, June 07, 2012

KAMBI YA UPINZANI YAIBANA SERIKALI

Na mwandishi wetu

Kambi Rasmi ya Upinzani imetaka maelezo ya kina ya kwa nini Serikali imeshindwa kutekeleza ahadi yake iliyoitoa Bungeni kuwa misamaha ya kodi itapunguzwa hadi asilimia moja ya pato la Taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Waziri Kivuli wa fedha na uchumi Bw. Kabwe zitto alisema Pia imerejea mwito wake wa kufutwa kwa mfumo wa posho za vikao pamja na kueleza kuwa bajeti ya mwaka 2011/2012 ilikuwa na changamoto kubwa ya utekelezaji.


"Serikali imependekeza bajeti ya sh. trioni 15 kutoka sh. 13 trillion. lakini ni dhahiri bajeti ya 2011/12 ilikuwa ina changamoto kubwa za utekelezaji. Serikali ieleze itawezaje kutekeleza bajeti ya sh.trillioni 15 katika bajeti mbadala ya 2012/2013," alisema Bw. Zitto.

Aliongeza kuwa Kambi ya Upinzani inaainisha maeneo ambayo Serikali inatakiwa kuyatekeleza.

Maeneo hayo ni kuendelea kushinikiza kupunguzwa kwa misamaha ya kodi hadi asilimia moja ya Pato la Taifa. Hadi sasa misamaha ya kodi ni sawa na misaada yote kutoka nchi wahisani, sh. trioni 1.03 ni sawa na asilimia tatu ya Pato la Taifa.

Pia kambi hiyo imeitaka Serikali kuelekeza rasilimali fedha kwenye maendeleo vijijini hasa kujenga miundombinu kama barabara za vijijini na umeme vijijini.

"Kuelekeza fedha za kutosha kukarabati Reli ya Kati na kufufua njia za Reli za Tanga, Moshi na Arusha, kuongeza wigo wa kutoza tozo la ujuzi ambapo sasa waajiri wote walipe ikiwemo Serikali na mashirika ya umma. Pia kupunguza tozo hili hadi asilimia nne, ambapo 1/3 itaenda VETA na vyuo vya Ufundi na 2/3 itaenda Bodi ya Mikopo ili kukabili changamoto ya mikopo kwa wanafunzi," alisema Bw. Zitto.

Maeneo mengine ni kushusha kima cha chini cha kodi ya mapato (PAYE) hadi asilimi tisa ili kuwezesha wananchi wa hali ya chini kubaki na fedha za kutumia na kukuza uchumi.

Lingine ni kuongeza mapato ya ndani na kupunguza mikopo ya kibiashara kwa kuhakikisha mapato ya ndani yanafikia asilimia 20 ya pato la taifa, kuongeza nguvu za kisheria na udhibiti ili TRA ikusanye mapato zaidi kwenye kampuni za simu na kwenye shughuli za uchimbaji wa madini, mafuta na gesi.


Bw.Zitto alisema kuwa wataishinikiza serikali kupunguza /kufuta kodi kwenye bidhaa za vyakula kwa muda maalum ili kushusha mfumuko wa bei.

Pia watato fursa kwa wafanyabiashara kuagiza mchele nje ya nchi bila kutoza kodi kwa kipindi cha miezi mitatu ili kupunguza makali ya kupanda kwa vyakula.

"Kambi ya upinzani itaendelea kufuatilia kwa karibu suala la kukua kwa deni la Taifa ambalo limefikia hadi sh. trilioni 22 na kutaka ukaguzi maalum kuhusu akaunti ya Deni la Taifa,"alisema Bw. Zitto na kuongeza;

"Kambi ya upinzani itawekeza kusimamia kwa karibu suala la matumizi yasiyo na tija ya Serikali hasa kwenye magari na posho mbalimbali na kuwa fedha nyingi zitumike kwa miradi mikubwa ya maendeleo ili kukuza ajira."

Alisema kuwa kuweka mfumo mpya wa elimu kwa kushirikisha sekta binafsi katika kutopa elimu kwa ubora zaidi ikiwemo kuundwa kwa chombo cha udhibiti wa elimu.

Pia kutoka vipaumbile na unafuu vya kikodi kwa viwanda vya ndani vinavyotumia malighafi za nchini hasa za kilimo na zenye kuongeza ajira kama korosho pamba na mkonge.



No comments:

Post a Comment