Friday, June 08, 2012

BAJETI MIUNDOMBINU YAPETA


KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imepitisha makadilio ya bajeti ya sh. bilioni 70.1 zilizotengwa kwa ajili ya Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia katika kipindi cha bajeti ya mwaka 2012/2013

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Bw. Peter Selukamba, alisema kuwa kati ya fedha hizo, sh. bilioni 39.8 zimetengwa kwa ajili ya maendeleo na zaidi ya sh. bilioni 30  ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida.

"Mtakubaliana nami kwamba kiasi kilichotengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida ni kidogo kuliko kiasi cha maendeleo, hivyo nasema kwamba tumepiga hatua pamoja na kwamba zipo changamoto tunazokumbana nazo,"alisema Bw. Selukamba.

Alisema changamoto hizo ni pamoja na bajeti ya sh. bilioni  64  za mwaka jana, ambapo wizara haikupata kiasi hicho chote badala yake ilipata  asilimia 46.5, hivyo ni mategemeo ya kamati hiyo kuwa Serikali itakamilisha bajeti hiyo kabla ya kuanza kwa bajeti nyingine.

Alisema kuwa kamati imekataa ombi la ongezeko la sh. nne katika gharama ya upigaji simu na kuisifu wizara hiyo kwa unafuu wa gharama zilizopo hivi sasa.

"Tumewapa maagizo kuwa wahakikishe mtandao unakuwa zaidi hadi kufika kwenye wilaya zote hata zile mpya, kushusha bei za intaneti ili mawasiliano yawe rahisi nchini, gharama kuendelea kuwa za chini ili kila mwananchi aeze kupata  mawasiliano," alisema.
          


No comments:

Post a Comment