Thursday, May 17, 2012

ACHA KUPARAMIA MAPENZI HAYANA MWENYEWE

KUTAMBUA mtu mwenye mapenzi ya kweli, utamjuaje mtu mwenye mapenzi ya kweli ni asilimia kubwa ya watu kushindwa kutofautisha mtu anayekupenda kweli na anayekutamani. Wengine wengi wameingia mkenge hasa wageni katika uwanja huu wa mahaba ukiambiwa unapendwa basi unachanganyikiwa na kusahau maneno matupu hayajengi nyumba. watu wengi wamekuwa wakitumia neno hili kama mtego wa kumpata mtu, kwa kujifanya anakupenda sana na nahau nyingi za mapenzi ambazo hukuziba masikio na kuona nani kama wewe na meseji tamu za mapenzi
Siku zote mtafutaji ana lugha tamu ya mapenzi na kabla ya kutamka lolote lazima atangulize nakupenda sana na kuongezea ajuavyo. hii si mara moja watu wameingia mkenge pale wanapoambiwa wanapendwa na kukubali mara moja bila ya kujiuliza, lazima ujielewe na kuutambua mwili wako kwani ukiupeleka vibaya lawama ni juu yako. Usiwe mtu wa kutoa maamuzi haraka haraka pale unapoambiwa unapoambiwa unapendwa hakuna hata siku moja mtu anayekutaka kimapenzi akuambie anakuchukia.
Jaribu kufikiria kabla ya kutenda na kuona kauli hii ina maana gani. Mwanadamu anamaamuzi tofauti na mnyama anayetumia nguvu bila ya mafanikio katika uchunguzi nimegundua watu wengi hupima kwa macho ya kuangalia alivyo, na asemalo unashindwa kuchukua muda wa kufikiria na kutoa maamuzi ya haraka bila kuangalia maamuzi yako yanafaida au hasara kwa vile amekuambia anakupenda na maneno matamu


Neno nakupenda sio mapenzi kamili bali tabia ya mtu na kuonyesha kweli anakupenda kwa dhati. Naakupendaye huwa hana haraka ya kufanya ngono hufuata taratibu zote ili mradi kujenga ukweli moyoni mwako. Na hii kutokana na kuwa na uhakika wewe ni wake hana wasiwasi kwa kutanguliza ngono mbele lakini ukiona umekutana na mtu na kutanguliza ngono baada ya neno nakupenda huyo hakupendi bali anakutamani. Tumekuwa tukitumia neno nakupenda kama kiwakilishi cha ujumbe wa mapenzi na si penzi kamili na mapenzi ya kweli ni ya vitendo na si maneno anayekupenda utamjua tu wala hajifichi.

 Ni mpole mwenye huruma anayekujali, muaminifu na mtu aliyemuwazi mwenye kukupa uhuru wa kumjua kiundani ili kuondoa wasiwasi
Mapenzi mengi ya siku hizi yamekuwa ya usiri na mipaka kama kweli anakupenda kwa nini akudanganye kwa nini akuwekee mipaka ya kumjua, ukimuona mpenzi wako msiri si muwazi mwenye mipaka ya kumjua lakini mdomoni kwake kuna kila nahau za kimapenzi na kulitamka neno nakupenda kama kiwalishi Huyo si mkweli wala hana mapenzi ya kweli bali amejificha nyuma ya neno nakupenda kuwa makini na watu hawa

No comments:

Post a Comment