Tuesday, March 27, 2012

Simba Ilivyoitesa Es Satif bao 2 - 0

 Wachezaji wa Simba wakimpongeza Boban baada ya kuifunga bao la pili timu hiyo kwenye mechi iliyochezwa jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini DSM, jumapili 25/03/2012

 Waheshimiwa nao walikuwepo, kutoka kushoto ni Samwel Sitta, Fredrick Sumaye, Said El Mamri, Zitto Kabwe, Aden Rage, na Juma Kapuya walikuwepo kushangilia Simba siku hiyo.

Emmanuel Okwi akipiga kichwa kujaribu kufunga goli katika mechi hiyo, huku ulinzi ukiwa umeimarishwa katika goli la Es Satif ya Algeria.

 Mwinyi Kazimoto akigombea mpira wa juu na captain wa timu ya Es Satif, Mourad Delhoum katika mechi hiyo ambapo Simba ilishinda bao 2 - 0

 Beki wa timu ya Es Satif, Smain Diss(5) aliyekabidhiwa kibarua cha kumbana Felix Sunzu, akitekeleza jukumu hilo, huku Boban (kulia) akichomoka kuelekea langoni, Simba ilishinda 2 - 0

 Golikipa wa Es Satif, Mohammed Benhamou akijaribu kumpooza Felix Sunzu baada ya kutendewa madhambi wakati akijaribu kufunga goli kwenye mechi hiyo.

 Hapa ndio mashabiki walivyojitokeza kwenye mtanange huo.

Kocha wa Simba, Milovan Cirkovic akifurahia ushindi baada ya kumalizika kwa mechi hiyo.

No comments:

Post a Comment