Mkutano wa Mbegu, Zanzoibar Beach Resort Hotel
(Picha zote na Ikulu ya Zanzibar)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Shein,(katikati)akiangalia mbegu za aina mbali mbali za mpunga
kutoka kampuni ya mbegu ya Vibha,Nchini India,katika maonesho ya biashara za mbegu,wakati wa mkutano wa siku tatu kuhusu mbegu kwa nchi
za Afrika ulioanza jana katika ukumbi wa Hotel Zanzibar Beach Resort,nje ya Mji wa Unguja,(kutoka kulia) P Vidya Sagar,Mkurugenzi
Mkuu na Mwenyekiti wa Vibha Seeds,Patrick Ngwediagi,Mwenyekiti wa Umoja wa Jumuiya za Wafanya Biashara wa Mbegu wa Afrika (12 AFSTA
CONGRESS 2012),na Waziri wa Kilimo wa Serikali ya Muungano Prof Jumanne Magembe,(kushoto)
Baadhi ya wajumbe kutoka Nchi mbali mbali wa mkutano wa siku tatu kuhusu mbegu kwa Nchi za Afrika (12 AFSTA CONGRESS 2012),wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Shein,(hayupo pichani) akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo ulioanza jana katika ukumbi wa Hotel ya Zanzibar beach Resort Nje ya Mji wa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na washiriki wa Mkutano wa siku tatu wa Mbegu kwa nchi za Afrika ,( 12 AFSTA CONGRESS 2012) alipokuwa akiufungua mkutano huo jana katika ukumbi wa Hotel ya Zanzibar Beach Resort,nje ya Mji wa Unguja.
No comments:
Post a Comment