Wednesday, March 14, 2012

Airtel Yazindua 3.75G, Internet Yenye Kasi Kuliko Zote Tanzania

  Meneja Masoko wa Airtel Bw Salim Madati akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya huduma mpya ya 3.75G katikati uzinduzi uliofanyika leo katika makao makuu ya Airtel Morocco ambapo sasa wateja wa Airtel wataweza kupata huduma ya internet iliyo ya kasi na kuwapatia ufanisi Zaidi katika shughuli zao za kila siku.
 
  Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bw Sam Elangallor akionyesha jinsi gani huduma ya 3.75 inavyoweza kutoa huduma ya internet iliyo ya kasi na kuwawezesha wateja wa Airtel kufanya video call wakati wa  uzinduzi wa huduma ya 3.75 iliyofanyika makao makuu ya Airtel na kuhudhuriwa na waandishi wa habari , wakishuhudia (kulia) ni mkurungezi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya na (kushoto )ni Meneja masoko Salim Madati.

  Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bw Sam Elangallor na mkurungezi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya  kwa pamoja wakionyesha jinsi gani huduma ya 3.75G  ilinavyoweza kuwawezesha wateja wa Airtel kupata huduma ya internet yenye ubora na kasi zaidi kwa watumiaji wenye simu zenye uwezo wa kutumia internet ikiwa ni pamoja na  kufanya video call wakati wa halfa fupi ya uzinduzi wa 3.75G  iliyofanyika makao makuu ya Airtel Morocco. 
 
  Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Bi Beatrice Singano Mallya akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma ya 3.75G uliofanyika leo katika makao makuu ya Airtel Morocco ambapo sasa wateja wa Airtel watapata internet yenye ubora na kasi  zaidi  , Pichani ni Mkurugenzi wa Airtel Sam Elangallor
Mkurugenzi wa Airtel Sam Elangallor akiinua modem na kumkabidhi Mwandishi wa habari kutoka TBC Jane John aliyejishindia modem wakati wa uzinduzi wa huduma ya 3.75G iliyofanyika makao makuu ya Airtel na kuhudhuriwa na waandishi wa habari, wakishuhudia ni baadhi ya wafanyakazi wa Airtel

No comments:

Post a Comment