Haya ndio inasemekana makazi ya baadhi ya wazee ambao wanaidai serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mafao yao baada ya Jumuiya hiyo kuvunjika mwaka 77. Inasemekana wanashindwa kurudi makwao na hatimae kuweka kambi karibu na stesheni ya treni jijini Dar es Salaam mpaka watakapolipwa madai yao.
Kama picha inavyoonyesha wanaishi kama ombaomba na hayo yamekuwa maisha yao kwa zaidi ya miaka miwili sasa. Swali ni je, Serikali haiwaoni hawa, na kama inawaona inampango gani nao? shida ni moja wote tunapita hapo mara nyingi tu na hakuna hata anaejisumbua hata kuwasaidia wazee hao, isitoshe maofisa husika sijui kama kuna wanalopanga kufanya. Inawezekana kabisa wote tukistaafu hivi ndivyo tutakavyokuwa?
Duh. . . pamoja na kwamba hatutaki kuzeeka ili yasitukute kama hayo lakini hatuna ujanja, itabidi siku moja wote tuwe wazee kama tutaishi muda mrefu. ila tusiwasahau wenzetu kiasi hichi, hao wazee inakuwa kama hawana familia au ndugu wa kuwatunza au hata serikali basi ichukue jukumu japo la kuwaheshimu hata kama hawawezi kuwalipa. ni maoni yangu tu.
No comments:
Post a Comment