Thursday, March 17, 2011

Yaliyo tokea mitaani kwa ufupi

Mtoto wa mtaani akiomba kwa mtindo wa kipekee jana katika barabara ya Bibi Titi, siku hizi ombaomba wamebadili style, wanawatumia watoto kukusanya mapato alafu wazazi wanafanya mrejesho mwisho wa siku chini ya miti. Hii inamaanisha kuwa watu wazima ombaomba wamepungua badala yake watoto ndo wanaongezeka

Mtaji wa maskini. . . muendesha guta akiangaika na mzigo pamoja na tajiri yake kama mzigo jana jioni katika barabara ya Kawawa,  Magomeni lango laJiji.

Jamaa yetu mwenye sarakasi ndani ya kazi, kijana huyu alionekana kwenye blog hii wiki iliyopita, jana tena alkamatwa na kamera akiwa anashusha mteremko wa Mlalakuwa na mzigo wake kama anavyoonekana


No comments:

Post a Comment