JANA TULIANDIKA KUHUSU WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA TANO, HUU NDIO MWENDELEZO WAKE
Kawambwa amewataka wanafunzi ambao hawataki kujiunga na kidato cha tano katika serikali atoe taarifa mapema kwani wamebaini asilia 20 ya wanafunzi wanaopangwa hawaripoti kwani kuna shule 303 zisizokuwa za serikali zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 16,000 wa kidato cha tano ambapo masomo yataanza Aprili 3, mwaka huu.
P i a w a z i r i Kawambwa amewataka wakuu wa shule binafsi kupeleka orodha ya wanafunzi na masomo wanayosoma ili kuweka taarifa sahihi za wanafunzi walioacha nafasi.
Wakati Kawambwa akitangaza matokeo yameibua hisia tofauti kutokana na kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha nne mwaka jana ambapo wengi walifeli hasa wa shule za kata na kusababisha matokeo kuwa mabaya.
Lakini takwimu zinaonyesha kuwa waliopata nafasi ya kuingia kidato cha tano mwaka huu ni wengi ukilinganisha idadi ya waliojiunga kidato cha tano mwaka jana
No comments:
Post a Comment