Friday, March 25, 2011

Kusoma Uingereza haitakuwa rahisi tena

Kutokana na ugumu wa maisha katika dunia ya tatu, watu kutoka katika mataifa hayo wanajitahidi kutumia fursa nyingi ili waweze kufika nchi za ulaya. Kwa kuliona hilo fursa moja wapo ni kwenda masomoni, kwa kuliona hilo serikali ya uingereza imetoka na mkakati mpya ambao maisha hayatakuwa marahisi tena
Sheria hizo ni pamoja na kupata viza, jinsi ya kuishi na kufanyakazi nchini humo na hata fursa mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwa wanafunzi wanaosoma uingereza. Kwa mujibu wa mtandao wa BBC, Sheria za kupata viza za wanafunzi nchini Uingereza zinatarajiwa kuwa ngumu zaidi
Waziri wa mambo ya ndani Theresa May alisema viza za wanafunzi hazitumiwi inavyotakiwa na "wengi wamekuja hapa kufanya kazi na si kusoma". Hii ni baada ya kuibuka wasiwasi kuwa mbinu za kuingia nchini humo kwa minajil hiyo hutumiwa kiudanganyifu
Mpango huo utapunguza idadi ya wanafunzi mpaka kufikia robo ambayo ni takribani 80,000
Waziri kivuli wa wizara ya mambo ya ndani Yvette Cooper alionya sheria hazitakiwi kuharibu idara zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni tano kwa mwaka.
Bi May aliliambia bunge kuwa matumizi mabaya ya viza za wanafunzi yamekuwa "ishara ya mfumo wa uhamiaji uliotumiwa vibaya".

Sheria za lugha
Sheria ngumu zilizowekwa ni pamoja na mwanafunzi kutakiwa kuzungumza lugha ya Kiingereza.
Bi May alisema alitaka kumaliza tatizo ambapo wale wanaojifanya wanafunzi hufika kwenye uwanja wa ndege wa Uingereza na kushindwa hata kutaja masomo wanayotarajia kufanya.
Pia utaratibu utazidi kubanwa kwenye kuwaruhusu wanaolelewa na mwanafunzi huyo kujiunga naye Uingereza- na idadi ya miaka ya wanafunzi kutoka nje kukaa Uingereza baada ya kumaliza masomo yao itapunguzwa.
Katika kukabiliana na wasiwasi wa viza za wanafunzi kutumiwa vibaya na wahamiaji wa kiuchumi, kutakuwa na kiwango maalum cha saa za kufanya kazi kwa wanafunzi kutoka nje.
Awali vyuo vikuu vilionyesha wasiwasi wa kupoteza wanafunzi kutoka nchi za nje kutokana na sheria kali za kuomba viza.
Vikwazo vingi vinawalenga wanafunzi walio katika vyuo vya watu binafsi badala ya vyuo vikuu.
Hata hivyo Bi May aliwaambia wabunge kwamba "njia kama hiyo" ya kusoma kupitia vyuo vikuu vitalindwa, iwapo tu vyuo vikuu vitawadhamini wanafunzi.


No comments:

Post a Comment