Wednesday, March 23, 2011

Gaddafi achimbia kwenye handaki, analindwa na askari 40


TRIPOLI,Libya

KIONGOZI wa Libya  Kanali Muammar  Gaddafi  inasemekana kuwa amejificha ndani handaki  ya siri  chini ya ardhi huku akiwa kwenye ulinzi mkali wa  askari wapatao  40 wakiongozwa na walinzi wake ambao ni wanawake.

  Kwa muujibu wa tovuti ya Mirror ya wingereza,inadaiwa ni kutokana na kuwa kiongozi huyo hajaonekana hadharani tangu Jumamosi wakati yalipoanza mashambulizi ya kwanza kutoka vikosi maalumu vya Uingereza huku kukiwepo taarifa nyingine zinazodai kuwa amekimbilia katika mji wa Sabha  ambao upo jangwani wenye watu wapatao 130,000 ambao wote wanamtii kiongozi huyo.


Kwa mujibu wa taarifa hizo, Kanali Gaddafi alichimbia chini ya ardhi muda mfupi kabla ya mashambulizi hayo kuanza hali ambayo ilimlazimu kuzungumza na kituo cha televisheni ya taifa mwishoni mwa wiki kwa njia ya simu badala ya kuonekana mbele ya kamera.


Pamoja na umaarufu wake wa kulindwa na askari wanawamke ambaye uvaa mavazi ya jeshi na viatu vyenye visigino virefu, inaelezwa kuwa kwa sasa Kanali  Gaddafi amezungukwa  na askari watiifu kutoka Chad, Niger na Ulaya ya Mashariki  ili kumpa ulinzi pande zote.

Wataalamu wanaeleza kuwa kiongozi huyo alichukua uamuzi wa kuzungumza na televisheni ya taifa kwa njia ya simu kutokana na isingekuwa rahisi kufahamu mahalia alipo.

Lakini hata hivyo pamoja na kujificha huko,nchini za Magharibi zinadai kuwa ataachia madaraka wakati wowote kutokana na kuwa ni wazi siku zake zinahesabika.

Taarifa hiyo ya Mirror imekaririwa ikisema bado inasemekana kiongozi huyo ameukimbia mji wa Tripoli ili kukwepa mashambulizi hayo ya anga yanayofanywa na washirika wa nchini za Magharibi lakini idadi kubwa ya wanaye ndiyo wamebaki nchini humo ili kusaidia kuendesha nchi.

Miongoni mwa watoto waliobaki katika mji mkuu huo ni pamoja na aitwaye Khamis,(32) ambaye anaripotiwa kufa baada ya makazi ya kiongozi huyo yaliyopo Bab al-Azizia kushambuliwa na kaka yake Saif al-Islam, (38) ambaye anasadikika bado yupo katika mji mkuu na ambaye ndiye anaendelea kuratibu shughuli za kifamilia.


Mataifa hayo ya Magharibi yanaeleza kuwa endapo atakuwa ameondoka kimya kimya ama kuuawa inatarajiwa kuwa wakazi katika mji wa  Tripoli na maeneo mengine ya Mashariki mwa Libya yatakuwa huru kuendeleza mapambano dhidi ya utawala wake.

Hata hivyo Kanali Gadafi amejitokeza jana na kutoa cheche kali kwa mataifa ya Marekani, Uingereza na Ufaransa na kudai kuwa Libya itayashinda mataifa hayo.


No comments:

Post a Comment