Monday, March 19, 2018

ZIMBABWE KUFANYA UCHAGUZI MWEZI WA SABA, 2018

Na Mwandishi Wetu
Immamatukio Blog.

Rais Emmerson Mnangagwa (pichani) wa Zimbabwe ametangaza jumamosi kuwa uchaguzi wa kwanza nchini humo wa Rais na Wabunge tangu kuondolewa madarakani Rais aliyeitawala Zimbabwe muda mrefu Robert Mugabe utafanyika mwezi julai.

Uchaguzi huo utakuwa ni jaribio la uongozi mpya uliotwaa madaraka mwaka jana novemba baada ya jeshi kulazimisha kujiuzulu kwa Mugabe (94). Pia itakuwa ni mara ya kwanza kufanyika uchaguzi bila sura ya Mugabe katika karatasi za kupigia kura toka mwaka 1980, ambapo nchi hiyo ilipopata uhuru toka kwa Mwingereza.

“Kama taifa, chama na serkali tunatarajia uchaguzi wa amani, uwazi na utulivu mwezi julai mwaka huu” alisema Mnangagwa mbele ya vyombo vya habari baada ya kukutana na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa jumamosi usiku.

Mnangagwa mwenye umri wa miaka 75, alisema uchaguzi huo utakuwa huru na usio na vurugu za aina yoyote kama zilivyokuwa zikitokea katika chaguzi za nyuma, sababu ambazo zilisababisha nchi hiyo kuingia katika uhusiano mbaya na nchi za magharibi.

“Nimeshakutana na vyama vyote vya siasa ambapo kwa pamoja tumekubaliana kuwa na uchaguzi wa amani” aliongeza Mnangagwa

Mnangagwa atangaza tarehe rasmi ya uchaguzi na kualika waangalizi kutoka nchi za Ulaya, ambao waliozuiliwa wakati wa utawala wa Rais Mugabe. Gazeti la wiki linalomilikiwa na serikali la Sunday Mail limesema timu ya awali ya uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya inatarajiwa kuingia nchini Zimbabwe leo(jumatatu).

Mkuu wa msafara kutoka Umoja wa Ulaya nchini Zimbabwe, Phillipe Van Damme, ameliambia gazeti hilo kuwa watakutana na Rais, viongozi wa siasa na vyama vya siasa pamoja na Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe.

Taarifa ya kwanza ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Robert Mugabe iliyotoka wiki iliyopita ikisema kuwa utawala wa Emmerson Mnangagwa “sio halali” na “umelaaniwa”







No comments:

Post a Comment