Mwanamke mwenye umri wa miaka 20 amekamatwa baada ya kusambaa video katika mtandao wa facebook ikionesha akimlazimisha mwanae wa mwaka mmoja kuvuta bangi. Brianna Ashanti Lofton (pichani) alikamatwa jumatano wiki hii na kufunguliwa mashtaka mawili ya unyanyasaji watoto pamoja na kukutwa na bangi.
Katika video hiyo ya kusikitisha, mkono wa mtu mzima unaonekana ukiwa umeshikilia kile kinachoonekana kuwa kipisi cha bangi akimwekea mtoto mdomoni. Mtoto huyo anaonekana kuvuta na kisha kutoa moshi.
Polisi walishtushwa na video hiyo baada ya msamaria mwema huko Rochester, New York, nchini Marekani kuweka kipande cha video mtandaoni, ndipo vyombo husika viliweza kufuatilia na kumtambua mama huyo na kisha kumkamata.
Polisi wanasema mtoto yuko salama na mama yake anashikiliwa. Taarifa ya polisi iliwashukuru wakazi pamoja na wote walioposti video hiyo mtandaoni kitendo ambacho kilisaidia kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo.
“tunashukuru sana kila mmoja aliyeisaidia polisi kumpata mama aliyeonekana katika video akimvutisha mwanaye. Asante kwa kujitolea kwenu, mtoto yuko salama na mama anashikiliwa na polisi” polisi iliandika katika mtandao wa facebook .
Mtoto yuko ustawi wa jamii huku mama yake akishikiliwa kwa kukosa dhamana ya dola laki moja. Lofton alishakamatwa mara nne katika kipindi kimoja katika matukio tofauti ikiwa ni pamoja na udhalilishaji.
picha ikimuonesha mtoto anavutishwa bangi
No comments:
Post a Comment