PICHA JUU: Muonekanao wa E-Passport zilizotolewa mapema mwaka huu.
Na Mwandishi Wetu.
KAMPUNI ya De La Rue ambayo ilishindwa kwenye zabuni ya E-Imigration ambapo ingetengeneza e-passport, e-Visa, e-Imigration nchini Tanzania imepata pigo jingine baada ya mkataba wake kusitishwa na Serikali ya Uingereza ya kuendelea kutengeza hati za nchi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Aliance News imesema kuwa kampuni ya De La Rue ilikuwa na mkataba na Uigereza wa miaka 10 lakini nchi hiyo imeamua kuvunja mkataba kati yake na kampuni hiyo. Imefahamika lengo la Serikali ya Uingereza kuvunja mkataba huo wa kutengenezwa hati za kusafiria ni kutokana na gharama kuwa kubwa za utengenezaji wa hati hizo na hivyo kuamua kuipa zabuni kampuni ya French firm Gemalto.
"Hati mpya za kusafiria za Uingereza hazitatengenezwa tena na kampuni ya De La Rue ambayo ndio iliyotengeneza hati zitumikazo kwa sasa. "Hivyo hati hizo mpya za rangi ya blue ambazo zitatumika baada ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya zitatengenezwa na kampuni ya French firm Gemalto.
Kubadilika kwa rangi ya hati hiyo kunatafsiriwa kuwa ni alama ya kurudi kwa nguvu ya Uingereza, umesema mtandao uliotoa taarifa hizi. Pia taarifa zinaeleza kuwa Kampuni ya De La Rue inafikiria kukata rufaa baada ya kukosa na kushindwa katika zabuni ya kutengeneza hati hizo mpya. Kampuni hiyo imeripotiwa ikidai haikuridhishwa kwa kupoteza zabuni hivyo hivyo inaweza kukata rufaa kutokana na uamuzi huo wa Serikali ya Uingereza.
Hata hivyo Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni ya De La Rue, Jitesh Sodha amesema kitendo hicho kimesababisha hisa za kampuni yao kutoka asilimia 14 ya Jumanne ya wiki hii hadi kufikia asilimia 0.4 jana Machi 22 ya mwaka huu. "Tumechukizwa na kitendo cha Serikali ya Uingereza kusitisha mkataba wetu wa kutengeneza hati za kusafiria za nchi hiyo wa miaka 10 kwani ulikuwa mkataba unamalizika Julai mwakani.
Hivi karibuni katika uzinduzi wa E-Passport, Rais Dk. John Magufuli amesema kuwa kuna wajanja awali walipanga kuutekeleza mradi huo kwa gharama kubwa kiasi cha dola za kimarekani milioni 226 ambazo ukizibadili kwa Dola moja sawa na shilingi 2245 mradi huo ungegharimu shilingi za kitanzania bilioni 507.
Rais Magufuli alisema baada ya kugundua ujanja huo, alivituma vyombo vya dola kufuatilia na kubainika mradi huo unaweza kutekelezeka kwa gharama nafuu na za kawaida ambapo baadae mradi umeonyesha kutelekezwa kwa dola milioni 57.8 sawa na bilioni 129 za kitanzania na hivyo kuliokolea taifa upotevu ambao ungeweza kujitokeza wa zaidi ya shilingi bilioni 380.
Moja ya kampuni ambayo ilikosa zabuni ya kutengeneza hati mpya ya kusafiria nchini Tanzania ni De La Rue na moja ya sababu ilikuwa ni kiasi kikubwa cha fedha ambazo walihitaji lakini Serikali iliwashtukia na kuamua kutoa zabuni kwa kampuni nyingine iliyotengeza kwa gharama nafuu. Hata hivyo vyanzo vya kuaminika kutoka Serikali ya Tanzania vilibanini mambo mazito yaliyoibuka baada ya kubainika kampuni hiyo kuhonga mamilioni ya fedha ili kupata mradi wa hati za kusafiria na uhamiaji kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment