Na BBC
Utafiti huo wa Marekani umebaini kwamba kemikali muhimu katika mafuta hayo hupiga jeki homoni za kike na kuharibu homoni za kiume. Mafuta ya mimea hiyo hupatikana katika bidhaa tofauti kama vile sabuni, mafuta ya kujipaka mafuta ya kuosha nywele pamoja na na bidhaa za kutengeza nywele.
Pia ni maarufu sana katika bidhaa za kuosha mbali na matibabu. Kiongozi wa utafiti huo, J.Tyler Ramsey kutoka taasisi ya kitaifa kuhusu mazingira ya sayansi ya afya katika jimbo la Carolina Kaskazini alionya watu kutahadhari wakati wa utumizi wa mafuta hayo.
''Jamii yetu huona mafuta hayo ya asilia kuwa salama. Hatahivyo humiliki kiwango kikubwa cha kemikali na ni sharti yatumiwe na tahadhari kwa kuwa baadhi yao husababisha uharibifu wa homoni''.
Visa kadhaa vya tatizo la kumea matiti miongoni mwa wanaume vimeripotiwa kutokana na utumizi wa mafuta hayo yenye manukato.
Baada ya kusitisha utumizi wa mafuta hayo tatizo hilo huisha lenyewe. Utafiti wa awali uliofanywa na Daktari Kenneth Korach - ambaye alichunguzwa kutokana na utafiti huo ulibaini kwamba mafuta ya mti wa Lavender na ule wa chai ulikuwa na ishara za kuharibu homoni zinazodhibiti tabia za kiume ambazo zinaweza kuathiri kubalehe na ukuwaji.
Utafiti mpya uliangazia kemikali nane muhimu kati ya 100 zinazotumika kutengeza mafuta . Kemikali nne zilizokaguliwa zilipatikana katika mafuta yote huku nyengine zikipatikana katika mafuta hayo yenye manukato.
Zilijaribiwa katika seli za saratani miongoni mwa binadamu katika maabara ili kupima mabadiliko.
Watafiti walibaini kwamba mafuta hayo yamekuwa yakipiga jeki homoni za kike na kuharibu zile za kiume.
''Mafuta ya Lavender na yale ya mchai yanasababisha madhara ya kimazingira na yanafaa kuchunguzwa'' , alisema bwana Ramsey. Kemikali nyingi zilizojaribiwa hazikuwa na madhara mabaya.
Tahadhari ya kutumia mafuta hayo.
Tahadhari lazima ichukuliwe unapotumia mafuta ya Lavender na yale ya mchai.
Usijipake mafuta ambayo hayajakuwa majimaji katika mwili wako moja kwa moja
Usitumie mafuta yasio majimaji kwa watoto walio chini ya miaka mitatau.
Iwapo ni mjamzito lazima upate ushauri wa daktari wako kabla ya kutumia mafuta hayo.
Iwapo mafuta hayo yatatumika vyema ni salama kwa familia nzima.
Prof Ieuan Hughes, ambaye ni profesa wa magonjwa ya watoto katika chuo kikuu cha Cambridge alisema kuwa matokeo hayo yamethibitisha a ni kwa nini mtu binafsi anayetumia mafuta hayo yalio na kemikali hizo humea matiti.
Madhara dhidi ya homoni za kiume huwa hayatarajiwi na haiwezekani kuzungumzia bila data.
Vijana walio tajiri zaidi duniani
Wanawake matajiri zaidi duniani 2017
Ni kweli kwamba sio watu wote wanaotumia mafuta hayo huathirika hivyobasi ni wazi kwamba kuna watu ambao ni rahisi kuathiriwa na kemikali za mafuta hayo ama pengine wanatumia bidhaa hiyo kupitia kiasi.
Alisema kuwa tahadhari inafaa kuangazia utumizi wa mafuta hayo. Amesema kuwa madhara ya muda mrefu ya utumizi wa mafuta hayo hatahivyo hayajulikani.
Bado hakuna ushahidi kamili kuthibitisha utafiti huo kwamba mafuta ya lavender na yale ya mchai husababisha matiti kumea miongoni mwa wavulana na tafiti za ukaguzi wa utafiti huo zinafaa kufanywa zaidi.
No comments:
Post a Comment