Monday, August 21, 2017
UBER YAZINDUA HUDUMA YA MADEREVA NA WASAFIRI KUCHATI KWA KUTUMIA PROGRAMU HIYO
Dar es Salaam Tarehe 21 Agosti 2017…Kampuni ya Uber nchini Tanzania imetangaza zana mpya maarufu kama “Kuchati Ndani ya Programu” inayowawezesha madereva na wasafiri kuandikiana ujumbe kwa kutumia programu hiyo bila malipo.
Kinyume na hapo awali ambapo madereva na wasafiri wangetumia Ujumbe Mfupi (SMS) au kupiga simu, zana hii inaleta unafuu kwa madereva na wasafiri hivyo basi kuwapunguzia kadhia ya gharama za kupiga simu sambamba na kuharakisha mawasiliano bila kuondoka kwenye programu ya Uber.
Maboresho haya ni juhudi endelevu za Uber na yanalenga kuimarisha wigo wa wasafiri na madereva wanapotumia programu ya Uber.
Zana hii mpya ni rahisi sana kuitumia. Msafiri anapoita gari, kuna kitufe cha ‘Kuwasiliana’ kwenye menyu inayoonekana chini ya skrini. Wasafiri wanaweza kuwaandikia ujumbe madereva, na madereva vivyo hivyo. Ujumbe utaonesha kwamba umepokelewa baada ya kuutuma.
Kwa upande mwingine, madereva watakiri kwamba wamesoma ujumbe kwa kugusa kwenye programu ya Uber ili watume ujumbe wa ‘bomba’. Ili wasijichanganye barabarani. Aidha wasafiri na madereva wanaweza kuona kama ujumbe wao waliotuma umesomwa.
Meneja Msimamizi wa Uber nchini Tanzania Bw. Alfred Msemo amehoji kwamba, “Kila safari nzuri huanza pale msafiri anapochukuliwa kwa gari, kwa hiyo tunajituma kutafuta mbinu za kumchukua msafiri bila usumbufu wowote kwa msafiri au dereva. Kipengele hiki cha Kuchati kitakuwa afueni kwa wasafiri na madereva wanapotaka kuwasiliana ili kusaidiana kutafuta mwafaka wa changamoto za safari kama vile, kufungwa kwa barabara au kutoa maelezo ya mahali walipo.”
Kadhalika, kipengele hiki kinatoa njia mbadala ya wasafiri na madereva kupiga simu wanapotaka kuwasiliana. Hata hivyo, ili mtu atumie kipengele hiki anatakiwa awe anatumia toleo la sasa la program ya Uber.
“Huu ni mwanzo tu wa mchakato wa kuimarisha huduma za kutuma ujumbe moja kwa moja kwenye programu ili kufanikisha wigo wa mawasiliano yasiyo na changamoto kwa wateja wetu, na kuwasaidia kuwasiliana katika ulimwengu wa utandawazi na ulimwengu halisi” amenukuliwa Bw. Msemo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment