Thursday, August 10, 2017

TWA YAZINDUA MWONGOZO, USHAURI NA MAFUNZO KWA WANAWAKE AFRIKA


Rais taasisi isiyo ya serikali ya wanawake wenye mafanikio Tanzania (Tanzania Women of Achievement….TWA) Irene Kiwia (Kulia) akiongea na hadhara wakati wa kuzindua zana ya taasisi hiyo itakayotumika kiubunifu kufundisha wasichana na wanawake nchini, uzinduzi huo umefanyika sambamba na mkutano wa taasisi ya Graca Machel Trust unaoendelea jijini Dar es Salaam.

Rais taasisi isiyo ya serikali ya wanawake wenye mafanikio Tanzania (Tanzania Women of Achievement….TWA) Irene Kiwia (Kulia) akiongea na hadhara wakati wa kuzindua zana ya taasisi hiyo itakayotumika kiubunifu kufundisha wasichana na wanawake nchini, uzinduzi huo umefanyika sambamba na mkutano wa taasisi ya Graca Machel Trust unaoendelea jijini Dar es Salaam.

Tarehe 09 Augst 2017, Dar es salaam, Tanzania: Taasisi ya Tanzania Women of Achievement (TWA), leo wamezindua jukwaa la kidijitali la kutoa mwongozo, ushauri na kujifunza kwa ajili ya wasichana na wanawake Afrika ambalo linapatikana kwenye mtandao na application ya simu lijulikanalo kama Twaa.

Jukwaa la ushauri la Twaa ni matokeo ya kazi endelevu za taasisi ya TWA katika programu za kujengea uwezo wanawake na wasichana zilizoanza mwaka 2009, zikiwa na malengo ya kuboresha maisha, kukuza fursa na kusaidia wanawake nchini Tanzania kufanikiwa ambao mwishoe watasaidia katika maendeleo ya jamii, nchi na bara kwa ujumla.
Jukwaa hili limeandaliwa kwa ajili ya kuunganisha, kukutanisha na kuwajengea uwezo wasichana kwa kuwawezesha kuchagua washauri kutoka katika orodha kubwa ya wanawake wenye ujuzi katika nyanja mbalimbali; na kujifunza masomo yaliyoandaliwa kwa ajili ya wasichana wa karne ya 21 katika nyanja za Afya, Ubunifu, Maendeleo ya Biashara, Maendeleo Binafsi, afya ya uzazi, haki, fasheni, urembo na mengine mengi.

Jukwaa la Twaa lina vijengea uwezo vingi ikiwa ni pamoja na kutoa msaada wa ushauri nasaha kutoka kwa wataalamu wa saikolojia, kuweka mipango na utaratibu wa kutekeleza majukumu ili kuwasaidia wasichana kuweka na kutimiza malengo yao kimkakati zaidi pamoja na kuwapa nafasi wasichana kuelezea kazi zao na kuhamasishana wao kwa wao.

Akiongea katika uzinduzi uliofanyika sambamba na kongamano la Women Advancing Africa lililoandaliwa na Graca Machel Trust jijni Dar es Salaam, Irene Kiwia, Mwanzilishi na Rais wa TWA alisema kwamba jukwaa la Twaa ni kama system ya GPS ambayo inasaidia kuwapa wasichana mwongozo wa maisha. Jukwaa hili litasaidia kuwezesha ukuaji wa ufahamu wa wasichana kwa kuboresha ujuzi wao, kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa kiwango cha juu na kuwasaidia kutambua uwezo wao kamili. Twaa inaziba pengo lililopo ambapo wanawake wanataka kulipa fadhila kwa kuwanyanyua wengine lakini wanakabiliwa na changamoto kwa kukosa muda kwaajili ya mawasiliano ya ana kwa ana kutokana na kuwa na majukumu mengi katika jamii. Na wasichana kote Afrika wanatafuta washauri wa kuwaongoza na kuwajenga lakini wanakabiliwa na changamoto ya namna ya kuwapata.

Jukwaa hili linapeleka kazi za TWA nje ya mipaka ya Tanzania, kwenda Afrika ambako taasisi hiyo inataka kupanua ushiriki wake. "Nina furaha kuongoza ubunifu ambao utaunganisha wanawake na watoto wa kike wa Afrika. Kwa fursa ambazo pia ndio changamoto zinazokabili Afrika, nina imani kuwa suluhisho liko katika takwimu, wingi wetu ndio silaha yetu. Kizazi kipya cha Afrika ni jibu katika kuziba mwanya wa ukuaji wa maendeleo uliopo kwa sasa. Sio tu kwamba Africa ni bara lenye idadi ya watu inayokuwa kwa kasi zaidi duniani, pia inakadiriwa kuwa litakuwa ni bara lenye watu wenye umri mdogo zaidi duniani kufikia mwaka 2035. Inakadiriwa kuwa Afrika itakaribia takribani nusu ya idadi ya watu ya dunia nzima kufika miongo miwili ijayo. Sasa huu ndio mtaji mkubwa sana wa bara hili na muda wa kukilea, kukiwezesha na kukiwekea misingi ya mahusiano kizazi cha Afrika ni sasa". Alieleza zaidi Kiwia.

Bi. Sadaka Gandi, Mshauri maarufu, mwanasaikoloji na Mwenyekiti wa TWA amesema ana lenga kuona wanawake viongozi katika Afrika wanainua jukwaa hili kulipeleka mbele na kulitumia ipasavyo kuwapa ushauri wasichana. "Twaa inawapa wanawake suluhisho la uhakika na lenye ufanisi la kuwawezesha wasichana, kubadilisha jamii na kubadilisha bara. Ni jukwaa linalowapa wanawake vinara nafasi ya kuwekeza binafsi kwenye jamii kama shukurani, kitu ambacho wanawake wengi wanakipenda. Tunatazamia kuwa jukwaa hili litaanzisha utamaduni wa kujifunza miongoni mwa wasichana, na vile vile kusaidiana. Kuna fursa nyingi sana nzuri ndani ya wanawake na wasichana wa Afrika, tunatazamia kuona maisha ya wasichana yanaboresheka na kuleta athari chanya Afrika zinazotokana na jamii ya wanawake waliowezeshwa.

Jukwaa hii ilianzishwa kwa ushirikiano na Shule Direct, taasisi ya kijamii ambayo inatoa vifaa vya mafunzo kwa njia ya kidigitali kwa wanafunzi Tanzania na Afrika nzima. Inapatikana kwenye play store ya android katika kundi la application za Lifestyle, na vilevile inapatikana kwenye mtandao kupitia www.twaa.co.tz.

Hii ni mara ya kwanza ambapo Shule Direct imejiingiza katika ubia na taasisi nyingine kwa ajili ya kupanua teknolojia yake katika kuwawezesha wanawake kuziba pengo la kusaidiana ambapo ni muhimu katika maendeleo yao binafsi na ya kitaaluma. "Kama taasisi inayoamini katika nguvu ya elimu kwenye kuibua vipaji, tunafuraha kushirikiana na TWA katika kutengeneza jukwaa hili la kipekee linalosaidia jinsi wanawake wanavyoungana, wanavyoshiriki na kujifunza. Nilivutiwa na kile ambacho TWA inatetea ambacho ni kupanua fursa na kuhakikisha kujifunza kunakuwa ni sehemu muhimu ya mafanikio ya wasichana. Wasichana wanapaswa kushika hatamu, kumiliki fursa na kulitumia jukwaa hili kwa ajili ya maendeleo yao.







No comments:

Post a Comment