Thursday, August 10, 2017

KAMPUNI YA NETWORK LTD YAZINDUA DROO KUBWA YA MILIONI 60


PICHANI:Mratibu wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Sebastian Maganga akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo Pichani) kuhusiana na mchezo wa bahati nasibu ya Tatu Mzuka, wakati wa uzinduzi wa mchezo huo wa kubahatisha nchini mapema jijini Dar es salaam (picha na ImmaMatukio Blog)

Na Mwandishi Wetu

Tatu Mzuka ni mchezo mpya wa jackpot uliobuniwa mahsusi kubadilisha maisha ya watu. Tatu Mzuka ni rahisi kucheza kwa kutumia simu ya mkononi, na kushinda ni baada ya kila lisaa limoja baada ya kucheza.

Kucheza Tatu Mzuka unahitaji kuchagua namba zako tatu za bahati, kati ya 0 na 9 kwa kufanya muhamala kwenye simu ya mkononi, linganisha namba mbili ili kujiongezea nafasi ya kushinda mara mbili, au linganisha namba tatu na ushinde mara 200.

Akieleza sababu ya kutumia namba tatu, Mratibu wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Sebastian Maganga alisema, “tumezungukwa na namba,, inaweza kuwa siku yako ya kuzaliwa, namba ya jezi ya mchezaji unayempenda au kumbukumbu yoyote hivyo tunaamini kila mtu anazo namba angalau tatu za bahati, sasa fikiria kutumia namba yako ya bahati kujishindia mamilioni ya fedha.”
Balozi wa Tatu Mzuka, Mussa Hussein akitambulisha Tatu mzuka kwa waandishi wa habari

Unaweza kubeti kuanzania Tsh 500 mpaka Tzsh 30,000 na kujiwekea nafasi ya kushinda mpaka Tzsh milioni 6 ndani ya lisaa. Kubeti na Tatu Mzuka ni kupitia huduma za fedha kwa njia ya mtandao, hivyo hutahitaji kufanya usajili wowote. Fedha utakazoshinda pia zitatumwa moja kwa moja kwenye simu yako.

“Kila unapobeti unaingia moja kwa moja kwenye droo ya wiki iitwayo Mzuka Jackpot, na droo hii inakupa nafasi ya kuwa milionea, hivyo basi kwa kila Tzsh 500 unayobeti kwenye Tatu Mzuka, unapata nafasi moja ya kuingia kwenye droo ya Mzuka Jackpot,” alieleza Maganga.

Aliongeza kuwa, kila ticket ya Tatu Mzuka inakuwa na viashiria vyenye herefu 6 zanazokuingiza kwenye droo ya Jackpot, hivyo ukibeti Tzsh 500, herufi zako zinaingizwa kwenye droo mara tatu, hivyo kukuongezea nafasi ya kushinda.

Muwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Daniel Wilson amewasihi watanzania kushiriki kwenye Tatu Mzuka na kuwa na nafasi ya kubadilisha na kuboresha maisha yako. Sera ya Tatu Mzuka ni uwazi, hivyo kila ushindi wa washiriki utachapishwa kwenye tovuti ya Tatu Mzuka (www.tatumzuka.co.tz).

Droo ya Jackpot itafanyika kila Jumapili na kurushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni vya TV1 na Clouds TV saa 3 kamili usiku na kutangazwa na mtanganzaji mashuhuri Mussa Hussein akiambatana na Antu Mandoza. Kila mshindi atakua na uhakika wa kushinda kati ya Tzsh milioni 2 na milioni 6, pamoja na kupata nafasi ya kujishindia milioni 30. Iwapo hakuna atakayeshinda milioni 30, basi wiki inayofata, kitita cha Mzuka Jackpot kitaongezeka mara mbili yake na kuwa milioni 60.

Ndani ya wiki moja tu tangu kuanza kwa Tatu Mzuka, wameshapatikana washindi zaidi ya 40,000, na kulipwa kiasi cha Tzsh milioni 100 kwa pamoja. Beti na Tatu Mzuka sasa upate nafasi ya kushinda Tzsh milioni 60 Jumapili hii.
 Mmoja wa waandishi wa habari akishiriki katika droo ya Tatu Mzuka wakati wa uzinduzi
 Balozi wa Tatu Mzuka, Shilole akishiriki katika mchezo huo wa kubahatisha mapema leo
 Baadhi ya Waandishi wa Habari waliokuwepo katika shughuli ya uzinduzi wa mchezo wa kubahatisha wa Tatu Mzuka mapema leo katika hoteli ya Serena






No comments:

Post a Comment