Na Tiganya Vincent
RS-TABORA WAKALA wa Barabara nchini (TANROADS) mkoani Tabora imesama kuwa tayari imeshaanza kutekeza hatua mbalimbali za maandalizi ya ujenzi wa barabara ambazo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliagiza ujenzi wake uanze mara moka wakati akiwa katika ziara ya mkoa huo.
Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Tabora na Meneja wa TANROADS Mhandisi Damian Ndabalinze kwenye kikao kazi kiliandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwa Mameneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini Tanzania(TARURA) wa mkoani humo.
Mhandisi Ndabalinze alisema kuwa katika barabara ya kutoka Kaliua hadi Urambo kazi za awali za kwa ajili ya kuanza maandalizi ya ujenzi inaendelea katika eneo la mradi.
Alisema kwa upande wa barabara ya ujenzi wa barabara ya Nyahua hadi Chaya yenye urefu wa Kilometa 84 wameshaanza hatua za awali baada ya Kuwait Fund ambaye ndio watoa fedha za mkopo wa ujenzi wa barabara hiyo kutokuwa na pingamizi.
Meneja huyo wa TANROADS Mkoa aliongeza kuwa hivi sasa wanachongojea ni ufunguzi wa zabuni ambayo itafanyika katika kipindi wiki moja ijayo ili kazi nyingine zianze.
“ Barabara ya Nyahua Chaya tumepata ‘no objection’ kutoka kwa Kuwait Fund….’consultant’ tulishafungua ile ‘technical’ sasa tunasubiri financial itafunguliwa tarehe saba Mwezi ujao kwa hiyo tunategemea tukishampata ‘Consultant’ mkataba utasainiwa kwa ajili ya kuanza kazi”alisema Ndabalinze.
Kuhusu tenda kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Pangale kupitia Kuga hadi Mpanda kwa kiwango cha lami , alisema kuwa zimeiva zinatarajiwa kufunguliwa tarehe sita mwezi ujao. Alisema kuwa ujenzi barabara hiyo kwa kiwango cha lami unatarajiwa kuanza mapema mwakani(2018).
Kwa upande wa barabara kutoka Ipole mkoani Tabora hadi Rungwe mkoani Mbeya yenye urefu wa kilimeta 172 Mshauri yuko katika eneo la mradi akiendelea shughuli mbalimbali za michoro na kuchukua vipimo mbalimbali ikiwemo aina ya udongo.
Alisema baada ya Mshauri kukamisha kazi hiyo itabaki shughuli ya kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami.
Mwezi uliopita Rais Magufuli alikuwa na ziara Mkoani Tabora ambapo alimwagiza Waziri, wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano kuhakikisha ndani ya Mwezi mmoja Mkandarasi wa ujenzi wa barabara ya kutoka Kaliua hadi Urambo ambayo ina umbali wa Kilometa 28 awe katika eneo la tukio.
Barabara nyingine ni ile ya Chaya hadi Nyahua ambayo ina urefu wa Kilometa 84 alisema ndani ya mwezi moja na nusu kandarasi iwe imeanza.
No comments:
Post a Comment