PICHANI: Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi kayombo akielekeza jambo wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua barabara ya Mawasiliano kuelekea Shule ya Sheria (Law school Of Tanzania)
Na Mathias Canal, Dar es salaam
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi kayombo Tarehe 6 June 2017 amekagua na kujionea hali ya ubovu wa barabara inayotoka Mawasiliano kuelekea Shule ya Sheria (Law school Of Tanzania) iliyopo katika Kata ya Sinza Jijini Dar es salaam.
Akizungumza mara baada ya kutembelea barabara hiyo katika ziara yake ya kikazi huku akiwa ameambatana na Kaimu Mkuu wa Idara ya Ujenzi na zima moto Ndg Goodluck Mbanga, Mkurugenzi Kayombo alisema kuwa matengenezo hayo yataanza hivi karibuni ili kurahisha huduma za kijamii kwa watumiaji wa barabara hiyo wakiwemo wananchi wa Mtaa wa Mawasiliano na Kata ya Sinza sambamba na wanafunzi wa Shule ya Sheria.
MD Kayombo alisema kuwa Fedha za matengenezo ya barabara hutolewa na Bodi ya Mfuko wa Barabara (Road Fund) ambapo lengo kuu ni kuhakikisha kuwa barabara zinapitika muda wote.
Kiwango cha matengenezo kimefikia wastani wa asilimia 90 kwa matengenezo ya aina mbalimbali hususani ya muda maalumu (Periodic maintenance), sehemu korofi (Spot Improvement), matengenezo ya kawaida (Routine maintenance) na ujenzi wa makalavati huku kiwango kikubwa pia kikitolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa barabara za lami.
Mwanzoni mwa mwezi Februari serikali ilizitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha wanasimamia sheria katika utendaji wao wa kazi pamoja na kufanya kazi kwa uadilifu, kutumia weledi wa taaluma zao katika kusimamia suala la usafi wa mazingira,yakiwemo masuala ya kudhibiti biashara holela, uegeshaji wa magari holela na ujenzi holela.
Mkurugenzi Kayombo alisema kuwa barabara hiyo itakuwa na urefu wa kilomita 1.2 hivyo kuhudumia wananchi wengi ambao wanataabika kwa adha ya ukorofi wa barabara hiyo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi kayombo akiwa na viongozi wengine wa shule ya Sheria Tanzania wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua barabara ya Mawasiliano kuelekea Shule ya Sheria (Law school Of Tanzania)

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi kayombo akiwasalimu wanafunzi wa Shule ya Sheria Tanzania wakiwa darasani wakati alipozuru Chuoni hapo wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua barabara ya Mawasiliano kuelekea Shule ya Sheria (Law school Of Tanzania)
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi kayombo akiwa na viongozi wengine wa shule ya Sheria Tanzania wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua barabara ya Mawasiliano kuelekea Shule ya Sheria (Law school Of Tanzania)
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi kayombo akiwa na viongozi wengine wa shule ya Sheria Tanzania wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua barabara ya Mawasiliano kuelekea Shule ya Sheria (Law school Of Tanzania)
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi kayombo akisaini kitabu cha wageni wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua barabara ya Mawasiliano kuelekea Shule ya Sheria (Law school Of Tanzania)
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi kayombo akiwa na viongozi wengine wa shule ya Sheria Tanzania wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua barabara ya Mawasiliano kuelekea Shule ya Sheria (Law school Of Tanzania)
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi kayombo akisikiliza maelezo mafupi kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo cha sheria Tanzania Dkt Willium Palanjo kuhusu changamoto ya ubovu wa barabara wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua barabara ya Mawasiliano kuelekea Shule ya Sheria (Law school Of Tanzania)
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi kayombo akizungumza na Viongozi wa Shule ya sheria Tanzania wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua barabara ya Mawasiliano kuelekea Shule ya Sheria (Law school Of Tanzania)
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi kayombo akiwa na Viongozi wa Shule ya Sheria Tanzania wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua barabara ya Mawasiliano kuelekea Shule ya Sheria (Law school Of Tanzania)
Kushoto ni Rais wa serikali ya wanafunzi Shule ya sheria Tanzania Ndg Emmanuel Nyanza, Dkt Clement Mashamba muhadhiri shule ya sheria Tanzanai, na Kaimu Mkuu wa Idara ya Ujenzi na Zimamoto, wakati wa ziara ya kikazi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi kayombo ya kutembelea na kukagua barabara ya Mawasiliano kuelekea Shule ya Sheria (Law school Of Tanzania)
No comments:
Post a Comment