Naibu katibu mkuu wa Klabu ya Gofu ya Jeshi ya Lugalo Kanali Rajabu Mwenyumbu akisalimiana na wachezaji wa gofu wa timu hiyo wanao tarajiwa kushiriki katika mashindano ya wazi Jijini Arusha mwisho wa Wiki hii.
Na Luteni Selemani Semunyu, JWTZ
TIMU ya Golf ya Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania ya
Lugalo imetamba kuendeleza ushindi katika mashindano ya wazi ya Mchezo wa golf
yanayotarajiwa kufanyika Jumamosi Oktoba 15 na 16 Jijini Arusha kwa kurejea na
Ushindi.
Hayo yamesemwa na Naibu katibu mkuu wa Klabu hiyo Kanali
Rajabu Mwenyumbu wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kwa Niaba ya
mwenyekiti wa Klabu hiyo Brigedia Jenerali Michael Luwongo wakati akiaga Timu
hiyo katika Uwanja wa Golf wa Lugalo Jijini Dar es Salaam.
Kanali Mwenyembu alisema maandalizi mazuri yamefanyika kwa
Timu zote ambazo zitashiriki mashindano hayo ambazo ni Daraja Senior
,A,B,C na Wanawake na watoto na kila daraja liko Vizuri na matumaini ni
makubwa.
“Nataka muendeleze nidhamu ya Kijeshi katika Michezo lakini
weledi katika mashindano ili kuhakikisha wanarejea na ushindi badala ya kuwa
washiriki katika mashindano hayo ambayo ni muhimu kwa viwango vya
Wachezaji” Alisema kanali Mwenyumbu.
Kwa Upande wake Mmoja wa Wachezaji hao Sara Damas
Alisema ni matumaini yake kuwa licha ya kuibuka na ushindi lakini pia
wanatarajia kupanda viwango vya uchezaji ukilinganisha na wakati uliopita.
Naye Mchezaji Juma Likuli alisema mazoezi
yaliyofanyika ni tofauti zaidi yaliyowajenga ipasavyo hali inayowapa matumaini
makubwa ya kuibuka ushindi.
Kwa upande wake Nahodha wa Klabu hiyo Kapteni
Japhet Masai alisema Jumla ya wachezaji 10 wanatarajiwa kwenda kushiriki
michuano hiyo wakiwemo wanawake watatu na wanaume Saba.
Aliongeza kuwa kikosi cha wachezaji hao Kitaongozwa na
Kapteni Amanzi Mangengule, Kapteni Japhet Masai, Kapteni Kibuna Shabani,
Juma Likuli,Noel Mheni,Nicolous Chitanda ,Michael Obare, Amina Hamisi,Sara
Denis na Sophia Mathias.
Kapten Masai aliongeza kuwa maandalizi yote yamekamilika na
kinachosubiriwa ni kurejea na Ushindi kama ilivyokuwa katika mashindano
yaliyopita ya Tanzania Open,Moshi Open na CDF Trophy ambayo klabu ya Lugalo
iliibuka washindi.
Naibu katibu mkuu wa Klabu ya gofu ya jeshi ya Lugalo Kanali Rajabu Mwenyumbu akizungumza na wachezaji wa gofu wa klabu hiyo ya jijini Dar es salaam wanao tarajiwa kushiriki katika mashindano ya wazi yanayotarajia kufanyika mwisho wa Wiki hii Jijini Arusha .(PICHA ZOTE NA LUTENI SELEMANI SEMUNYU)
No comments:
Post a Comment