Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John PombeMagufuli, leo tarehe 31 Oktoba, 2016 ameondoka nchini
kuelekea Nairobi nchini Kenya kwa ziara ya Kiserikali ya siku mbili nchini humo
kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Mwalimu Julius Nyerere, Rais Magufuli ameagwa na viongozi mbalimbali wa serikali
akiwemo Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
John Kijazi, Mkuu wa Mkoa wa Dar Es salaam, Paul Makonda na viongozi mbalimbali
wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
Mara baada ya kuwasili nchini
Kenya, Rais Magufuli atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais Uhuru
Kenyatta, na baadae atakwenda kutoa heshima katika Kaburi la Rais wa Kwanza wa
Kenya Hayati Mzee Jomo Kenyatta.
Mheshimiwa Rais pia anatarajiwa
kuhudhuria dhifa ya kitaifa atakayoandaliwa na mwenyeji wake Ikulu Jijini Nairobi.
Katika ziara hiyo Rais Magufuli
anatarajiwa kutembelea kiwanda cha maziwa cha
Eldoville kilichopo Karen Jijini Nairobi na pia kuzindua barabara mchepuko
(Southern By-pass) iliyopo Jijini humo.
Barabara hiyo ni moja kati ya miradi mikubwa ya barabara nchini Kenya, inayounganisha
maeneo mbalimbali ya Jiji la Nairobi kwa barabara za juu na chini.
Jaffar
Haniu
Naibu Mkurugenzi wa
Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar Es Salaam
31Oktoba, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Balozi wa Kenya nchini Mhe Boniface Muhia katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa tayari kwa safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili leo Oktoba 31, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea saluti toka kwa Inspekta jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa tayari kwa safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili leo Oktoba 31, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa tayari kwa safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili leo Oktoba 31, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipungia wakati akipanda ndege kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tayari kwa safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili leo Oktoba 31, 2016
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na viongozi wengine wakipunga mikono kumuaga Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati akianza safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili leo Oktoba 31, 2016
No comments:
Post a Comment