Wednesday, October 12, 2016
CHUMI AENDELEA KUTAFUTA WADAU WA KUISAIDIA SHULE YA MSINGI MAKALALA
Mkurugenzi wa TEA Joel Laurent katikati akiangalia darasa la Tehama Computer ambazo baadhi zilitolewa kama msaada na TEA kwa shule hiyo.
na fredy mgunda,Iringa.
MBUNGE wa jimbo la mafinga mjini cosato chumi amewataka wananchi kuendelea kujituma kufanya kazi wakati akitafuta ufumbumzi wa kero na changamoto mbalimbali za jimbo hilo jimpya.
Aliyasema hayo alipokutana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bw Joel Laurent katika Shule ya makalala yenye mahitaji maalumu huku lengo likiwa ni kumuonyesha mkurugenzi huyo jinsi hali ilivyombaya ya kitaalum na mazingira yalivyo magumu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu.
“Ninajitahidi kufanya kila kinachowezekana ili mradi kutatua changamoto za wananchi wa jimbo la mafinga na kuleta maendeleo kadili ninavyoweza” alisema chumi
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elim Tanzania Bw Joel Laurent alisema kuwa atatuma timu yake ya wataalam kwa ajili ya kufanya tathimini ya mahitaji ya miundombinu katika Shule ya Msingi Mchanganyiko ya Makalala iliyopo Mafinga.
Bw Laurent aliyasema hayo siku Alhamis alipoitembelea Shule hiyo kufuatia ombi la Mbunge wa Mafinga Mjini.
Mkurugenzi huyo alisema kwamba TEA pamoja na mambo mengine Ina wajibu wa kusaidia miundombinu na vifaa saidizi vya kufundishia na kujifunzia na kwamba Mwaka huu wataelekeza nguvu katika Shule za mahitaji maalum kama Makalala na kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Shule za kawaida.
Shule hiyo yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 48 wa bweni wenye ulemavu wa akili, wenye ualbno na wenye uono hafifu inakaribiwa na uhaba wa Bweni ambapo kwa Sasa wanafunzi wanalazimika kulala mpaka watoto Sita katika baadhi ya vyumba.
Naye mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Williamu alisema kuwa anaishukuru TEA kwa kuitikia wito wa kuitembele shule hiyo yenye mahitaji maalumu na kuomba serikali kuwapa ushirikiano kutatua changamoto za shule ya makalala sambamba na kuwaomba wada wengine kuendelea kuisadia shule hiyo.
Wiki iliyopita TEA ilitoa msaada wa vifaa visaidizi vya kusomea katika shule ya Ilboru sambamba na kukabidhi fimbo nyeupe mkoani Mbeya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment