Tuesday, August 09, 2016

RC MONGELLA AZUNGUMZIA ZIARA YA RAIS MAGUFULI MKOANI MWANZA

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (kulia) akitoa taarifa ya ujio wa Rais Magufuli mkoani Mwanza. Kushoto ni Katibu Tawala mkoani Mwanza, CP.Clodwig Mtweve.

Judith Ferdinand, Mwanza
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli, anatarajia kufanya ziara fupi ya kikazi mkoani Mwanza.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, leo amesema, Rais Magufuli atafanya ziara ya siku mbili kuanzia kesho agost 10 na 11, ambapo atapokelewa hiyo kesho wilayani Sengerema akitokea Chato mkoani Geita alikokuwa na mapumziko mafupi.

"Rais Magufuli atawasili kesho asubuhi katika mkoa wetu akitokea Chato mkoani Geita na ataanza ziara katika wilaya ya sengerema kwa ajili ya kuwasalimia wananchi, kuwapa taarifa za mikakati na maendeleo awamu ya tano pamoja na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi". Amesema Mongella.

Pia amesema hiyo kesho Rais Magufuli atasimama maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuwasalimu wananchi kabla ya kuwasili wilayani Nyamagana.

Ametanabaisha kwamba Rais Magufuli ataitimisha ziara yake kesho kutwa agost 11, kwa kukagua ujenzi wa daraja la watembea kwa miguu la Furahisha Jijini Mwanza, pamoja na upanuzi wa barabara ya Furahisha hadi Pasiansi ambapo ataweka jiwe la msingi katika ujenzi wa miundombinu hiyo.

Mongella amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi katika mkutano wa hadhara utakaofanyika kuanzia majira ya saa nanne mchana katika uwanja wa Furahisha ambapo Rais Magufuli atahutubia wananchi baada ya kukagua miradi hiyo ya ujenzi.


Mwanahabari akiuliza swali

Bonyeza HAPA Kusoma Zaidi.

No comments:

Post a Comment