Na Daud Magesa, Mwanza
WATUHUMIWA wawili wa ujambazi waliokuwa wakihusishwa na mauaji ya wauamini watatu katika Msikiti wa Rahman pamoja na unyang’aji katika maduka ya M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money Hamis Juma (38) mkazi wa Nyegezi ametoroka akiwa chini ya ulinzi wa polisi na mwingine Mohamed Bishof au Gunda Mika (31) amefariki dunia .
Mtuhumiwa huyo anadaiwa kuwatoroka polisi Julai 3 , mwaka huu majira ya saa 2:00 usiku katika eneo la mlima wa Kiloreli Nyasaka katika Manispaa ya Ilemela.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi, mtuhumiwa huyo liwatoka askari wa upeleelzi ambao aliwapeleka katika mlima huo kwenda kuwaonyesha maficho majambazi wenzake wanayotyatumia kujificha.
Alisema baada kufika eneo hilo majambazi wenzake walishituka na kuanza kufyatua risasi askari hao ambao walitaharuki na kisha kujibu mashambulizi hayo. Msangi alieleza kuwa wakati majambazi na askari wakiendelea kujibizana kwa kurushiana risasi mtuhumiwa huyo Juma alitumia mwanya huo kuwatoroka polisi na kutokomea usiku huo.
Katika mapambano hayo askari waliambulia kupata risasi iliyokuwa moja ikiwa kwenye chemba ya bunduki hiyo moja aina ya Short Gun iliyokatwa mtutu na kitako chake wake ambayo ilikuwa ikitumiwa na majambazi hao baada ya kuitupa na kutokomea ambapo msako na juhudi kubwa zinafanyika za kumsaka mtuhumiwa huyo.
Aidha, katika tukio jingine mtuhumiwa mwingine wa matukio hayo ya uporaji na mauaji ya waumini wa dini ya Kiislamu Mohamed Bishof au Gunda Mika (31) shombe wa Kiarabu amefariki dunia kutoka na majeraha aliyoyapata baada ya kuruka kutoka kwenye gari la polisi.
Mtuhumiwa huyo aliruka kutoka ndani ya gari hilo katika eneo la Kiloreli Nyasaka kwa nia ya kutoroka ambapo alianguka barabarani na kuumia kichwani na sehemu mbalimbali za mwili wake na alifariki wakati akikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza ya sekou Toure kwa matibabu. Wakati akijaribu kutoroka kwa kuruka kutoka kwenye gari la polisi na kuanguka
Mtuhumiwa huyo katika mahojiano na polisi alikiri kufanya uhalifu wa unyang’anyi wa kutumia silaha kwenye maduka ya kutoa huduma za kifedha pamoja na mauaji n wakati anakamatwa alikutwa kakiwa na vifaa vay kielektroni (electronic divice) alivyokuwa akivitumia kufanya uhalifu jijini na nje ya Jiji la Mwanza
Pia alikutwa akiwa na kompyuta mpakato waliyopora katika tukio la uporaji la Mei 5, mwaka huu huko Kishiri Centre mali ya Phares Gabriel ambaye walimjeruhi mguuni kwa kumpiga risasi na kupora kiasi cha fedha kisichojulikana.
Msangi alisema kuwa jeshi hilo linaendelea na msako dhidi ya watuhumiwa wanaodaiwa kuhusika katika matukio ya uporaji kwe nye maduka ya M-Pesa, TigoPesa na Airtely Money na kuhakikisha wanatiwa mbaroni.
No comments:
Post a Comment