Tuesday, July 19, 2016

RAIS MSTAAFU MWAI KIBAKI ATEMBELEA DARAJA LA MWALIMU NYERERE

Mwakilishi Maalumu wa masuala ya maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa Kenya Mwai Kibaki (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Maonesho ya Wiki ya Maji Afrika (Sylivester Matemu) wakati wa maonesho ya sita katika ya wiki ya maji Afrika yanayoendelea jijini Dar es salaam. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo.


Na Mwandishi Wetu

Mwakilishi Maalumu wa masuala ya maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa Kenya Mwai Kibaki ametembelea mabanda ya maonesho ya sita katika ya wiki ya maji Afrika yanayoendelea jijini Dar es salaam.

Katika tukio hilo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo amimweleza Mwakilishi huyo kuwa Tanzania imejipanga kuhakikisha kuwa hadi ifikapo 2020 iweze kufikisha maji kwa wananchi wote kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

Mhandisi Kalobelo aliongeza kuwa hatua hiyo itaifanya Tanzania kufikisha maji kwa wakazi wa mijini kwa asilimia 95 na kwa wakazi wa vijijini kw asilimia 85.

Aidha, katika hatua nyingine, Mwakilishi huyo alitembelea barabara iliyopewa jina la Mwai Kibaki inayoanzia eneo la Morocco hadi njia panda ya Kawe jijini Dar es salaam pia alitembelea na daraja la Mwalimu Nyerere linalounganisha eneo la Kigamboni kupitia bahari ya Hindi na eneo la katikati ya jiji la Dar es salaam.
Maonesho ya sita katika ya wiki ya maji Afrika mwaka huu yanayoendelea jijini Dar es salaam yanaongozwa na kaulimbiu inayosema “Kufikia lengo la Mendeleo Endelevu (SDGs) juu ya Usalama wa Maji na Usafi wa Mazingira”.          
Mwakilishi Maalumu wa masuala ya maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa Kenya Mwai Kibaki akisalimia na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo leo jiji Da es salaam.
Katibu wa Mwakilishi Maalumu wa masuala ya maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa Kenya Mwai Kibaki (katikati), Profesa Nick Wanjohi akifafanua jambo kwa mwakilishi huyo alipotembelea na daraja la Mwalimu Nyerere linalounganisha eneo la Kigamboni kupitia bahari ya Hindi na eneo la katikati ya jiji la Dar es salaam.

Mwakilishi Maalumu wa masuala ya maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa Kenya Mwai Kibaki (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi walioandamana kutembelea daraja la Mwalimu Nyerere linalounganisha eneo la Kigamboni kupitia bahari ya Hindi na eneo la katikati ya jiji la Dar es salaam.

(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)


No comments:

Post a Comment