TANGAZO MUHIMU
Kwa Wakazi wa Kata za Makurumla, Mburahati, Manzese, Mabibo Sinza, Ubungo, Makuburi, Kimara, Mbezi, Msigani, Saranga, Goba, Kibamba na Kwembe. Ninyi ni wakaazi wa Wilaya Mpya ya Ubungo.
Kwa kila aliye na kero, ninapendekeza tuanze na zile kero sugu na kubwa kubwa na kama hakuna basi hata zile za kawaida. Kwa miezi miwili kutoka sasa Mimi na watumishi wenzangu wa Wilaya yetu, tutasikiliza na kuharakisha utatuzi au ushauri stahili.
Utolewaji wa Huduma kwa wananchi Wilayani Ubungo unazingatia Sera ya "Mlango Wazi". Serikali Ubungo inasema "Tuambie Ukweli ili tutende haki na wewe upate Haki yako"
Tafadhali na shime wana Ubungo, tujulishane ujumbe huu, ili ndani ya muda mfupi Ubungo iwe Wilaya ya Tofauti, itakuwa ngumu mwanzo ila itakuwa uhalisia mapema zaidi tukishirikiana.
Unaweza wasiliana nami moja kwa moja kupitia 0786146700 (nisipopokea tuma ujumbe mfupi-SMS) au kwa Mwezi huu wa Julai fika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Tutakuwepo kuwasikiliza na kuwahudumia.
Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano amenituma niwatumikie na kuwahudumia kama Mtumishi na Kiongozi wenu.
Humphrey Polepole
Mkuu wa Wilaya UBUNGO
No comments:
Post a Comment