Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akizungumza na viongozi wa mfuko wa Abbott (Abbott Fund) kutoka nchini Marekani na wale wa Tanzania waliomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam kuzungumza naye kuhusu masuala mbalimbali ya uboreshaji wa huduma za Afya na Elimu kupitia program mbalimbali zinazofanywa na Mfuko huo nchini. Kutoka Kulia ni Makamu Mtendaji wa Rais wa Mfuko wa Abbott, Stephen Fussell na Makamu wa Rais Mwandamizi wa Mfuko wa Abbott (Abbott Fund Bi.Elaine Leavenworth (katikati).
Makamu wa Rais Mwandamizi wa Mfuko wa Abbott (Abbott Fund) Bi.Elaine Leavenworth (kulia) akimweleza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) juu ya namna Mfuko wa Abbott ulivyojipanga kuendelea kutekeleza Program mbalimbali nchini Tanzania zikiwemo za Matumizi ya Teknolojia ya kisasa katika utoaji wa Tiba, maabara za kisasa, dawa na vifaa vya mafunzo kwa wanafunzi wa masomo ya Sayansi.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akifurahia jambo na Makamu wa Rais Mwandamizi wa Mfuko wa Abbott (Abbott Fund) Bi.Elaine Leavenworth (kushoto) mara baada ya ujumbe wa viongozi wa mfuko huo kutoka nchini Marekani kumtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam.
Ujumbe wa viongozi wa mfuko wa Abbott (Abbott Fund) kutoka Marekani ukimsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla mara baada ya kumtembelea Ofisini kwake leo jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Mfuko wa Abbott (Abbot Fund) nchini Tanzania Andy Wilson akielezea utayari wa Mfuko huo katika kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazoikabili sekta ya Afya na Elimu nchini kupitia ufadhili wa Programu mbalimbali zinazofanywa na Mfuko huo kwa niaba ya Watu wa Marekani. Picha/ Aron Msigwa –MAELEZO.
No comments:
Post a Comment