Tuesday, June 28, 2016

WANAHABARI WATEMBELEA VIJIJI VINAVYO PAKANA NA HIFADHI YA TAIFA YA MILIMA YA MAHALE

Baadhi ya Wanahabri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale inayosifika kwa uwepo wa Sokwe Mtu.
Usafiri unaotegemewa katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale ni Boti na Mitumbwi .
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania ,Pascal Shelutete (Mwenye kofia) akiwa na Mkuu wa Idara ya Ujirani Mwema wa Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale ,Romanus Mkonda wakielekea katika vijiji vinavyopakana na Hifadhi hiyo,Wengine ni wmwandishi wa gazeti la Uhuru,Jackline Massano na kulia ni Mhariri wa gazeti la Jamhuri ,Mkinga Mkinga.
Wanahabari ,Said Mnekano maarufu kama Bonge wa Clouds fm,aliyesimama nyuma.akiwa na Asiraji Mvungi pamoja na muongoza watalii ,Rashid Omary wakiwa katika moja ya boti zinazotumika kama njia ya usafiri katika Hifadhi ya Taifa ya Mahale.
Waandishi ,Beatrice Shayo na Nora Damian wakijaribu kushuka kutoka katika boti.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akionozana na wanahabari kutembelea kijiji cha Nkokwa kinachopakana na Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale.
Ili kuwafikia wananchi maeneo mengine wanahabari walilazimika kuvua viatu na kupita katika maji.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAP A) akizungumza na wananchi katika kijiji cha Nkonkwa wilayani Uvinza.
Baadhi ya wananchi wanaounda vikundi vya wajasilaimali wakimsikiliza Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) Pascal Shelutete (hayupo pichani ) alipoongozana a wanahabari kutembelea vijiji vinavypakana na Hifadhi ya Taifa ya Miima ya Mahale.
Mkuu wa Idara ya Ujirani Mwema katika Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale ,MhifadhiRomanus Mkonda akizungungmza katika kikao hicho.
Kijana mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja akijaribu kusukuma chombo chake kwa kutumia kandambili wakati akisafiri katika ziwa Tanganyika.


Na Dixon Busagaga wa Michuzi blog aliyeko mkoani Kigoma.


No comments:

Post a Comment