Imeelezwa kuwa ipo haja kwa vituo vya Afya hapa nchini kuwepo na wataalamu ambao watasaidia kitaaluma kubaini, kutibu na kutathimini magonjwa yatokanayo na kazi.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) Masha Mshomba wakati wa mafunzo kwa madaktari yanayohusu kubaini na kutibu magonjwa yatokanayo na kazi.
Amesema kuwa kuna kila sababu ya vituo hivyo kuwe na wataalamu ambao watasaidia kutambua na kutibu magonjwa yaokanayo na kazi ili kurahisisha masuala ya ulipaji wa fidia.
Mshomba ameeleza kuwa suala la kutambuna na kubaini magonjwa yatokanayo na kazi ni la kitaalamu zaidi na ndio maana mfuko huo umeamua kutoa mafunzo hayo kwa madaktari.
"Mafunzo haya kwa madkatari yatawasaidia kufanya tathimini ya magonjwa yatonakayo na kazi ili wawe miongoni mwa washauri wa mfuko huo,pia mafunzo haya ya awamu ya kwanza yamewashirikisha Madaktari 93 kutoka mikoa ya Dar es salaama, Morogoro, Dodoma, Lindi, Mtwara na mikoa mingine ya Pwani.
Anaongeza kuwa mpango huo una lengo la kutoa mafunzo kwa madaktari 380 nchi nzima na kwamba yatatolewa awamu kwa awamu katika mikoa ya Arusha, Mwanza na Mbeya.
Kuhusu uchangiaji katika mfuko huo, Mshomba, alisema kuwa muamko wa uchangiaji ni mkubwa na umekuwa ukiongezeka siku hadi siku kadri elimu kuhusu mfuko huo inavyotolewa.
Kwa upande wake, Mjumbe wa Bodi ya Mfuko huo ambaye pia aliiwakilisha TUCTA, Rashmina Mbilinyi, alisema kuwa bodi ina hamu kubwa ya kuona mfuko huo unafanyakazi kwa ufanisi lengo likiwa ni kuwasaidia wafanyakazi wanaopatwa na majanga wakiwa kazini.
Amesema kwa sasa changamoto bado hazijapatikana kwa sababu mfuko huo utaanza rasmi kutoa mafao ifikapo Julai, mwaka huu na kwamba mpaka sasa makusanyo ni mazuri kwa kuwa waajili wengi wamehamasika katika uchangiaji.
Mafunzo yamedhaminiwa na Shirika la Kazi Duniani(ILO) kwa niaba ya Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi(WCF).
No comments:
Post a Comment