Monday, May 16, 2016

BUNGE LAHAIRISHWA LEO,SAKATA LA LUGUMI BADO GIZA NENE


                            
Bunge limelazimika kuahirishwa kwa muda baada ya msemaji wa kambi ya upinzani Bungeni kuhusu Wizara ya Mambo ya Ndani God bless Lema, kuitwa mbele ya kamati ya kanuni kufuatia kile kilichodaiwa kuwa hotuba yake ilikuwa na mambo yanayokinzana na kanuni za Bunge.

Ambapo kuitwa kwa Lema mbele ya kamati hiyo, kulifanya hotuba ya kambi hiyo ya upinzani kushindwa kuwasilishwa kwa wakati Kama ilivyokuwa taratibu, huku wabunge wa wote wanaotokana na CCM wakiitwa katika kikao cha dharura.

Awali kabla ya kutangaza kusitisha kwa shughuli za Bunge kabla ya wakati, Mwenyekiti wa Bunge Mussa Zungu ambaye ndiye aliyekuwa akiongoza Bunge leo, alimtaka Lema pamoja na kiongozi wa upinzani Bungeni kutoka bungeni na kwenda mbele ya kamati hiyo ya kanuni.

Akisoma tangazo mbele ya Bunge Zungu amesema kuwa kamati hiyo inapaswa kukutana ili kutafuta muafaka wa maudhui yaliyomo katika hotuba hiyo ya upinzani.

"Naomba kamati ya kanuni , Mheshimiwa Lema pamoja na kiongozi wa kambi ya upinzani, kukutana na kujiridhisha kuwa maudhuhi yaliyomo katika hotuba ya msemaji wa upinzani, yanakidhi masharti ya uendeshaji wa Bunge hili"

"Hivyo basi naagiza kamati ya kanuni ikutane Mara moja katika ukimbi wa spika, wakati tunaendelea na shughuli za Leo, na ikifika zamu yake kusoma hotuba ya upinzani wakati kamati ya kanuni haijamaliza muda wake ntatoa mwongozo utakaofuata"anasema Zungu

Hata hivyo tangazo ilo, lilizua mjadala na minong'ono ndani ya Bunge ambapo baadhi ya wabunge walisikika wakisema 'lugumi'.

Hata kabla shughuli za Bunge kuendelea,aliibuka kaimu kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni Mchungaji Peter Msigwa ambaye alisema kuwa hoja hiyo inaonesha wazi kuwa kambi inaelekezwa au kupangiwa cha kusema.

"Mheshimiwa mwenyekiti tunaomba tupate maelezo ya kina, taarifa za upinzani zinaandaliwa na kambi nzima, kwa hiyo ni maoni yetu sote, sasa tunashangaa kuona tunaanza kuingiliwa na kuambiwa cha kusema wakati inapaswa maoni yetu kuwasilishwa na kuja kujibiwa kwa hoja na Serikali "anaeleza Msigwa

Hata hivyo hoja yake ilijibiwa na Zungu ambaye amesema jambo ilo ni la kikanuni hivyo litapatiwa ufumbuzi wa kikanuni, na ni vyema wakaenda kuhudhuria kikao hicho kupata ufumbuzi.

Baada ya majibu hayo yalimfanya Mh. Lema na wajumbe wa kamati hiyo kuinuka kwa ajili ya kwenda katika kikao hicho, Bunge liliendelea ambapo Waziri wa Mambo ya Ndani Charles Kitwanga aliwasilisha hotuba ya makadirio ya bajeti ya Wizara hiyo.

Hotuba hiyo ya bajeti ya Kitwanga ilifuatiwa na maoni ya Kamati ya Bunge ya mambo ya nje, ulinzi na usalama kuhusiana na wizara hiyo ambayo ilisomwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Balozi Adadi Rajabu.

Katika maoni yake kamati hiyo mbali na mambo mengine, iligusia sakata la kampuni iliyopewa zabuni na jeshi la Polisi kwa ajili ya kusambaza mashine za kunakili alama za vidole ya Lugumi,ambapo kamati hiyo iliruka kuzungumzia jambo ilo.

Kwenye maoni yake kamati hiyo mbali na kudai kutambua uzito na umuhimu wa jambo hilo kufahamika, iliruka na kusema kuwa jambo ilo liliibuliwa na CAG na kwamba tayari lipo mbele ya kamati ya PAC.

"kwakuwa suala ili tayari inashughulikiwa na kamati ya PAC tunaomba jambo ili liachwe kwa kamati hiyo ili itafute ufumbuzi"anasema Balozi Rajabu

Mbali na Wizara na Kamati kutoa maoni yao na kusoma bajeti, kamati ya kanuni ilikuwa bado haijamaliza kikao chake na hivyo kulazimika kutolewa kwa hoja ya kuahirishwa kwa Bunge mpaka kipindi cha jioni.

Akitoa hoja ya kuwasilisha shughuli za Bunge kabla ya wakati, Mnadhimu Mkuu wa Serikali bungeni Jenista Mhagama alisema kuwa kwakuw kikao hicho hakijakamilisha kazi yakee Bunge ilo lisingeweza kuendelea hivyo kuomba liahirishwe mpaka Majira ya saa 10 jioni.

Zungu aliahirisha Bunge hilo, ambapo hoja ya kuahirishwa kwa bunge ilipokelewa kwa hisia tofauti na wabunge huku wa upinzani wakipiga kelele.

Tangazo la Zungu kuahirisha Bunge lilitanguliwa na tangazo la kuwataka wabunge wote wanaotokana na CCM kukutana katika kikao katika ukumbi ambao ulikuwa ukitumika hapo awali kuendeshea Bunge (ukumbi wa Pius Msekwa).

Baadhi ya Wabunge wakielekea Bungeni kwa ajili ya vikao vya asubuhi leo,kutoka kulia ni Waziri wa Habari,Tamaduni,Sanaa na Michezo,Mh.Nape Nnauye na kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum(CCM),Mh.Halima Bulembo.




No comments:

Post a Comment