* IDADI YA WATOTO WANAOINGIA LA KWANZA YAONGEZEKA
Serikali inaendelea na mazungumzo na wawekezaji wanaokusudia kuwekeza katika viwanda vya sukari ili kuongeza uwezo wa uzalishaji kwa ajili ya kukabiliana na upungufu wa bidhaa hiyo nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakati akijibu maswali ya papo kwa papo ya kila Alhamis.
Alisema kuwa lengo la mazungumzo ya kutaka viwanda viweze kuongeza uzalishaji wa sukari ili uweze kufikia tani 420,000 katika kipindi miaka minne ijayo na hivyo kupunguza uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi.
Mhe. Majaliwa alisema kuwa maeneo ambayo yametengwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vipya ya Sukari ni pamoja na Kigoma, Morogoro na Bonde la Rubada lilipo katika mto Rufiji.
Kuhusu kutojengwa kiwanda cha Sukari katika eneo la Bagamoyo , Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali ilikataa kuruhusu ujenzi wa kiwanda cha Sukari katika eneo hilo baada ya Kamati ya Bunge kushauri kuwa kisijengwe kwa sababu kingehatarisha uhai wa wanyama waliomo katika Mbuga ya Saadan kwa kuwa kingetumia maji mengi kutoka Mto Wami.
Mhe. Majaliwa alisema kuwa hali hiyo ingesababisha upungufu wa maji ambayo ni tegemeo kwa wanyama wa Mbuga ya Saadan yambao ni muhimu kwa sekta ya utalii nchini.
UPUNGUFU WA SUKARI.
Kwa
upande wa upungufu wa sukari nchini , Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali
imeagiza tani 70,000 kutoka nje ya nchi.
Alisema
kuwa mahitaji ya sukari ni tani 420,000 lakini zilizopo ni tani 320,000 na
kuwepo kwa upungufu wa tani 100,000.
Mhe.
Majaliwa alisema kuwa Bodi ya Sukari nchini ili kukabiliana upungufu huo
imeweka utaratibu wa uagizaji huo ili kuhakikisha Waagizaji wa Sukari nje wasije
wakaingiza sukari nyingi kinyume cha inayohitajika na hivyo kuathiri viwanda vya
hapa nchini.
Aliongeza
kuwa Bodi hiyo kwa kushirikiana Mamlaka
ya Mapato nchini (TRA ) itasimamia kuhakikisha kuwa sukari inayoingiza nchini
ndio inayohitajika.
Kuhusu
bei elekezi ya sukari , Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali inaweka kiwango ili
kumlinda mwananchi wa kawaida.
Alisema
kuwa bei hiyo zinazingatia gharama zote ikiwemo usafirishaji kutoka zinapoagizwa
na kumfikia mlaji.
WAZIRI MKUU APIGA MARUFUKU LUMBESA
Katika
hatua nyingine Waziri Mkuu amesema kuwa ni kosa kwa wanunuzi wa mazao ya wakulima
kununua mazao kwa vipimo visivyo halali ambavyo havikuidhinishwa na Wakala wa
Vipimo nchini.
Amewaagiza
viongoizi wote wa Halmashauri,Wilaya na Mikoa yote nchini kuhakikisha wakulima hawanyonywi
kupitia wananunuzi mazao kuliko vipimo halisi kama vile Lumbesa.
Mhe.
Majaliwa amewaagiza Kamati za Ulinzi na Usalama katika za mikoa na wilaya
kusimamia zoezi hili ili mkulima alipe kwa vipimo halali ambavyo ni kilo au
gunia liloshonwa kiwanda na sio lile liloongezewa kichuguu(lumbesa).
ELIMU YAONGEZA IDADI YA WATOTO WANAOINGIA LA
KWANZA
Kuhusu
suala la elimu bure, Waziri Mkuu amesema kuwa lengo ilikuwa na lengo la kumpunzia
mzazi mzigo wa ada ya shule za Msingi na Sekondari.
Mhe.
Majaliwa alisema kuwa ada hizo zilikuwa ni kati ya shilingi elfu 20 na elfu 70.
Amesema
kuwa sehemu imebebwa na Serikali ni pamoja na maji,ulinzi,umeme na gharama za
mitani mbalimbali.
Aidha,
Mhe. Majaliwa alisema kuwa baada ya mpango huo wa elimu bure kumekuwepo na
ongezeko kubwa na watoto waliondikishwa kujiunga darasa la kwanza mwaka huo na hivyo kusababisha changamoto ya upungufu wa
madawati na madarasa.
Alisema
kuwa Serikali inaendelea kuzifanyia changamoto hizo na kutoa wito wadau
mbalimbali kuungano mkono juhudi hizo za Serikali.
No comments:
Post a Comment