Monday, May 16, 2016

MAYUNGA KUZINDUA VIDEO NA AKON KATIKA FINALI ZA AIRTEL TRACE MUSIC STARS


Mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga akirekodi video yake na mwanamuziki nguli wa miondoko ya R& B Akon nchini Marekani.


Mwanamuziki nguli wa miondoko ya R& B Akon akiwa na Mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika mwaka Jana.


Na Mwandishi Wetu

Mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga anategemea kuzindua video yake mpya ijulikanacho kama “Please don’t go away” aliyoifanya na mwanamuziki nguli duniani Akon nchini Marekani

Nalimi Mayunga alipata nafasi ya kurekodi wimbo huo mara baada ya kuibuka kuwa mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika na kuwashinda washiriki wengi kutoka nchi 12 barani Afrika

Kibao hicho chenye mahadhari ya R& B kimeanza kupigwa au kuchezwa leo katika radio mbalimbali nchini wakati ambapo video yake inategemewa kuzinduliwa rasmi siku ya Ijumaa 20 Mei 2016 wakati wa finali za msimu wa pili wa shindano la Airtel Trace Star 2016 linalowashirikisha washindi watano bora ambao wanashindania kitita cha shilingi milioni 50 ikiwa ni pamoja na nafasi kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya AfrikaAirtel Trace Star yatakayofanyika hivi karibuni nchini Nigeria


Akiongea kuhusu wimbo wake na Akon, Mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga alisema “ kwa kweli namshukuru Mungu sana kwa kuniwezesha kufika mpaka hapa lakini pia nawashukuru Airtel kwa kunipa nafasi hii kubwa ya kuweza kurekodi wimbo na Mwanamuziki wa kimataifa Akon. Nafurahi sana sasa video hii iko tayari baada ya mashabiki wangu kuisubiri kwa muda mrefu. Natumaini nyimbo yangu itafanya vizuri ndani na nje ya nchi na kunipa fursa ya kuwa mwanamuziki nyota na hii ndio imekuwa ndoto yangu. Nawaomba watanzania waniunge mkono ili nyimbo zangu na muziki wangu uendelee kufanya vizuri.”

Aliongeza kwa kusema ”Napenda pia kuchukua nafasi hii kuwapongeza washiriki wa mwaka huu walioingia tano bora na kuwashauri waweke juhudi na nia ili waweze kujinyakulia ushindi na hatimae kutuwakilisha vyema katika mashindano ya Afrika na kurudi na ushindi nyumbani”. Aliongeza Mayunga

Naye Meneja uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando alisema , tunajivunia kuendelea kuwawezesha watanzania kuonyesha vipaji vyao ndani na nje ya nchi kupitia shindano hili la Airtel Trace Music Stars . Tunaamini video ya Mayunga itafanya vizuri ikiwa watanzania tutamuunga mkono Star wetu huyu, nachukua fursa hii kuwaomba wadau mbalimbali wa tasnia ya muziki kuisikiliza na kuipiga katika vyombo mbalilmbali kama radio, TV na klabu za muziki ili iwafikie mashabiki wengi”

Kufatia ushindi wake Nalimi Mayunga ameweza kupata mafunzo ya muziki toka kwa Akon pamoja na kurekodi kibao hicho kipya cha “Please don’t go away” na pia amepata nafasi ya kurekodi upya wimbo wake nchini South Afrika ujulikanao kama “Nice Couple”ambao unaendelea kufanya vizuri sana kwa sasa



No comments:

Post a Comment